Maandalizi ya sherehe za miaa 37 ya kuzaliwa kwa ccm

Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari
kwenye uwanja wa Sokoine ,ambapo alisema maandalizi yote yamekamilika
,majukwaa yamekamilika, uwanja umerekebishwa vizuri na vijana wa Halaiki
wamejiandaa vya kutosha tayari kwa sherehe ya kuzaliwa kwa CCM tarehe 2
Februari.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki hatua za mwisho za maandalizi ya mahala ambapo maandamano yatahitimishwa.

Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na vijana wa Halaiki
ambao watashiriki kuonyesha Halaiki kwenye kilele cha miaka 37 ya
kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi ambayo kitaifa yatafanyika mkoani Mbeya
tarehe 2 Februari.

Jukwaa
litakalotumika kwa burudani likiwa kwenye hatua za mwisho kufungwa
kwenye uwanja wa Sokoine ambapo Band ya TOT na wasanii wa vizazi vipya
wanategemewa kutumbuiza.
No comments:
Post a Comment