JK AHANI MSIBA WA QORRO
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombelezo
ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Karatu Waziri wa Kilimo na Ushirika
Serikali ya awamu ya kwanza, Mhe. Patrick Qorro (72) aliyefariki dunia
usiku wa kuamkia Jumamosi baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa
hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Mifupa ( MOI) jijini Dar es
Salaam.
Marehemu Qorro ambaye wakati wa Serikali ya awamu ya kwanza aliwahi
kushika nyadhifa mbalimbali, ikiwamo Waziri mdogo wa Kilimo na Ushirika
na baadaye kuwa waziri kamili wakati wa awamu ya pili, alikuwa
akisumbuliwa na tatizo la kuvuja damu kwenye mzunguko wa kichwa
kulikosababishwa na hitilafu ya figo.Kwa mujibu wa msemaji wa familia,
Bw. James Bwana, Marehemu anatarajiwa kuagwa rasmi kesho kabla ya
kusafirishwa Jumatano hadi Kijiji cha Mbulumbulu, wilayani Karatu,
mkoani Arusha kwa ajili ya mazishi.
:Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa marehemu Dkt Martha
Qorro na wanafamilia wengine nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa Karatu
Waziri wa Kilimo na Ushirika Serikali ya awamu ya kwanza, Mhe. Patrick
Qorro (72) aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Jumamosi baada ya kuugua
kwa muda mfupi na kulazwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha
Mifupa ( MOI) jijini Dar es Salaam.


No comments:
Post a Comment