WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MHE. MATHIAS CHIKAWE ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA NCHINI, JIJINI DAR

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(katika Jukwaa)
akipokea Salaam ya Utii toka Gadi Maalum ya Kijeshi iliyoandaliwa na
Maofisa wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) alipotembelea Ofisi za
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo Januari 23, 2014, Jijini Dar es
Salaam.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akikagua Gadi
Maalum ya Gwaride lililoandaliwa na Maofisa wa Jeshi la Magereza
alipotembelea Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo Januari 23,
2014 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mathias Chikawe akisalimiana na
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Gideon Nkana alipotembelea
Ofisi za Makao Makuu ya Magereza Nchini leo Januari 23, 2014, Jijini Dar
es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa taarifa
fupi ya hali ya Uendeshaji wa Magereza Nchini kabla ya kumkaribisha
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe kuongea na
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza alipotembelea Ofisi za Makao
Makuu ya Jeshi la Magereza leo Januari 23, 2014.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akiongea na
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani)leo Januari 23,
2014 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza(wa pili kulia) ni
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima(wa kwanza
kulia) ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak
Abdulwakil(wa kwanza kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John
Casmir Minja

Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakimsikiliza Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe alipotembelea na kuongea
na Maafisa Waandamizi wa Magereza wa Ofisi za Makao Makuu ya Magereza
leo Januari 23, 2014 Jijini, Dar es Salaam.Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza
No comments:
Post a Comment