Aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii na Sasa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi Amkabidhi Ofisi Rasmi Waziri Mpya Wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid na Naibu Wake Dkt. Kebwe S. Kebwe

Aliyekuwa
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hussein Mwinyi kushoto
akimkabidhi kitabu hicho Waziri Mpya wa Wizara hiyo Dkt. Seif

Naibu Waziri Dkt. Kebwe kulia, akikabidhiwa kitabu na Waziri Dkt. Mwinyi

Aliyekuwa
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii na sasa ni Waziri wa Ulinzi na jeshi
la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi (kushoto) akizungumza na
watendaji wa wizara hiyo (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya
ofisi na aliyekuwa Naibu Waziri wake na sasa ameteulikuwa kushika
nyadhifa ya Uwaziri Dkt. Seif Rashid (kulia), anayefuata ni Naibu Waziri
wa Wizara hiyo Dkt. Kebwe S. Kebwe.Makabidhiano hayo yamefanyika
kwenye ukumbi wa Waziri, wizarani hapo.

Waziri
wa Afya na Ustawi wa jamii Dkt. Seif Rashid (kulia) akizungumza na
watendaji wa wizara hiyo (hawapo pichani) na kutoa shukrani zake za
dhati kwa aliyekuwa Waziri wake Dkt. Hussein Mwinyi kwa ushirikiano
wake kipindi alipokuwa akiongoza wizara hiyo.

Waziri wa Ulinzi Dkt. Mwinyi akiteta jambo na katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jami, Charles Pallangyo.

Naibu
Waziri Dkt. Kebwe S. Kebwe akizungumza na watendaji wa wizara hiyo na
kuwataka kufanya kazi kwa ushirikiano na mahusiano mazuri ili
kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta hiyo

Mawaziri hao wakisaini vitabu vya makabidhiano ya Muundo na Utekelezaji wa Wizara

Mawaziri hao wakiwa kwenye picha ya
pamoja mara baada ya makabidhiano pamoja na watendaji wa wizara hiyo.
Wa kwanza kushopto waliokaa ni Katibu Mkuu, Charles Pallangyo, aliyekuwa
Waziri wa afya na ustawi wa jamii Dkt. Mwinyi, Waziri mpya wa wizara
hiyo Dkt. Seif nna wa mwisho kulia ni Naibu Waziri Dkt. Kebwe S. Kebwe.Picha zote na Catherine Sungura-Wizara ya Afya
No comments:
Post a Comment