Header Ads

Tamasha la Biashara kuanzishwa


01
Naibu Mkurugenzi Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Rashid Ali Salum akimkaribisha Waziri wa Wizara hiyo Nassor Ahmed Mazrui katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Chuo cha Maendeleo ya Utalii Maruhubi kuhusu Tamasha la Biashara la miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
 
Na Ali Issa, Maelezo
 
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazurui amesema nyezo muhimu ya kuendeleza Biashara ni kuanzisha na kuendeleza Tamasha la Biashara kwa ajili ya mauzo ya Bidhaa mbalimbali zinazo zalishwa viwandani, bidhaa za wajasairiamali, bidhaa za kilimo na huduma za biashara.
 
Hayo ameyasema leo huko Chuo cha Maendeleo na Utalii Maruhubi Zanzibar wakati alipokuwa na mazungumzo na wandishi wa Habari kuhusiana na Tamasha la Biashara la miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Amesema nchi nyingi duniani zimeanzisha matamasha ya biashara kwa lengo la kuhamasisha na kuendeleza biashara katika nchi zao na kupelekea kuinua uchumi wa nchi zao.
 
Amesema Zanzibar  hivi sasa imeona ni vyema na wao kuwa na utaratibu kama huo kila mwaka ili kuona  nayo inapiga hatua kubwa kibiashara na kuimarisha uchumi wake.

No comments:

Powered by Blogger.