Mamia Zanzibar wanufaika na huduma za NHIF
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima akisaini kitabu cha wageni katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya alipotembelea bandani hapo.
Naibu Waziri huyo akipata ushauri kutoka kwa wataalam baada ya kupima uzito, sukari na shinikizo la damu. 
Ofisa Matekelezo na Uratibu Ainess
Bamanyisa akitoa elimu kwa askari polisi waliohitaji ufafanuzi wa
huduma zinazotolewa na Mfuko.
………………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
MFUKO
wa Taifa wa Bima ya Afya umehudumia mamia ya wananchi wa visiwani
Zanzibar wamepata huduma za vipimo na ushauri wa kitaalam wa kuepukana
na maradhi yasiyoambukiza kwenye banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF).
Wakazi
hao ni wale waliofika kwenye maonyesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya
Mapinduzi ya Zanzibar yaliyomalizika visiwani humo jana.
Uongozi
wa mfuko huo umeweka huduma hizo ambazo zinatolewa bure katika maonesho
hayo kwa lengo la kuwasaidia wananchi kutambua afya zao na kuweza
kujikinga.
Vipimo vilivyotolewa katika banda hilo ni pamoja na vipimo vya urefu, uzito, shinikizo la damu na kisukari.
Mbali
na kuhudumiwa, Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko huo, Bw. Hamis Mdee ametoa
mwito kwa wananchi visiwani humo kujiunga na NHIF ili wawe na uhakika wa
kupata matibabu popote pale walipo Tanzania.
“Nitumie
fursa hii kuwaomba sana Wazanzibari kuona umuhimu wa kujiunga na huduma
zetu ili muweze kunufaika na mtandao mkubwa tulionao wa watoa huduma
nchi nzima, sisi ni binadamu hatujui ni lini tutakuwa wagonjwa na
tutakuwa wapi lakini hapa fedha unaweza ukawa huna kwa wkati huo hivyo
ni vyema ukawa mwanachama,” alisema.
Alisema
kuwa NHIF imesogeza huduma zake visiwani humo kwa kufungua ofisi ili
wananchi na wanachama waweze kupata huduma kwa uharaka na ukaribu zaidi.
Akizungumza
katika banda hilo, Ofisa Udhibiti Ubora wa NHIF, Dk. Ally Mvita alisema
idadi ya wananchi wanaofika kwa ajili ya vipimo hivyo iliongezeka siku
hadi siku.
“Hii
inatoa hamasa kwa wengine kuja kupima lakini pia tunawashauri wote
wanaofika bandani kwetu namna bora za kujikinga na magonjwa hayo
yasiyoambukiza,” alisema Dk. Mvita.
Awali
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Hamis Mdee alisema hiyo ni fursa kwa
wakazi wa visiwa hivyo kujua afya zao huku akiwataka kuwatumia vema
wataalam hao wa afya.
Kwa
mujibu wa Mdee lengo la NHIF ni kusogeza huduma kwa wananchi wote ili
kufikia malengo ya kuwafikia watanzania wote kwa kuwa afya ni msingi wa
maendeleo na uchumi imara.
Mfuko
huo unatoa mafao 11 kwa wanachama wake kupitia watoa huduma
waliowasajili katika kuhakikisha wanachama wao wanapata huduma bora za
afya waakati na mahala popote.
Baadhi
ya mafao yanayotolewa na NHIF ni gharama za upasuaji, kulazwa, vipimo,
dawa mbalimbali, matibabu ya macho, miwani ya kusomea, kinywa na meno,
mazoezi ya viungo, mafao kwa wastaafu, vifaa saidizi na ada ya
uandikishaji.
No comments:
Post a Comment