MAHMOUD THABIT KOMBO KUUNGURUMA LEO KWENYE MKUTANO WA HADHARA –BUYU PWANI

Na Andrew Chale, Zanzibar
CHAMA
cha Mapinduzi CCM, leo Januari 24, kinatarajia kufanya kampeni yake ya
tatu ya mkutano wa hadhara kwenye eneo la Buyu Pwani, katika kampeni za
Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki, ambapo mgeni rasmi wa kumnadi
Mgombea anatarajiwa kuwa, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa
Jumuiya ya CCM (UVCCM) na (MNEC), Ndugu. Shaka Hamdu Shaka.
Akielezea
mkutano huo wa tatu wa hadhara, unaotarajiwa kuwa majira ya Saa kumi
jioni, eneo hilo la Buyu- Chukwani, Mahmod Thabit Kombo , aliwaomba
wananchi wa Buyu kujitokeza kwa wingi ilikumsikiliza na kuzijua sera za
Chama katika kuwaletea maendeleo.
“Leo
Januari 24, nawaomba wananchi wa Buyu, kujitokeza kwa wingi
ilikusikiza sera , Ilani na mipango endelevu tuliyojipangia ndani ya
chama” alisema Mahmoud Thabit Kombo.
Aidha,
aliwaomba wananchi wa Buyu, ifikapo Februari 2, 2014 siku ya Jumapili,
wampigie kura ya NDIYO, ili awe Mwakilishi wao atakayeenda kuwatetea
kwenye Baraza la Wawakilishi, sambamba na kumaliza kero zinazowakabiri.
Baadhi
ya mambo, mbalimbali anatarajia kuzungumzia ikiwemo kero za maji,
elimu, kuwezesha vijana, akinamama na jamii nzima ya jimbo hilo la
Kiembesamaki, pindi watakapomchagua.
No comments:
Post a Comment