Ona Jinsi Naibu wa Sayansi na Teknolijia na mbunge wa Bumbuli-CCM January Makamba Alivyoung'uruma Kwenye Kongamano kubwa la siku moja la Umoja wa Madereva wa pikipiki Mwanza lililofanyika katika uwanja wa michezo wa Nyamagana

Kabla ya kongamano hilo
madereva hao wa bodaboda walifanya maandamano toka makao makuu ya ofisi
zao yaliyopo mtaa wa malango mmoja wilayani Nyamagana jijini Mwanza hadi
katika uwanja wa historia wa Nyamagana.

Wadau wa Bodaboda wakiingia uwanja wa Nyamagana.

Wakizidi kumiminika viwanjani hapo kuhudhuria kongamano lao.

Ndani ya uwanja wa Nyamagana madereva wa Bodaboda wamejitokeza kiasi cha kutosha.

Naibu wa Sayansi na Teknolijia
ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli mhe. January Makamba akiingia katika
uwanja wa Nyamagana kushiriki kongamano la Bima ya Afya kwa waendesha
pikipiki maarufu kama Bodaboda wa mkoa wa Mwanza.

Naibu wa Waziri wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia January Makamba akihutubia
----
Audio-Gsengo
Audio-Gsengo
NAIBU wa Waziri wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia January Makamba
ametaka ujio wake Jiji la Mwanza usihusishwe na Kampeni za chini kwa
chini za Urais bali ni kutekeleza ombi la Umoja wa waendesha pikipiki
Mkoa wa Mwanza kuwasaidia kupata Bima ya Afya baada ya kuwawezesha
kupata pikipiki 1745 za FEKON na si vinginevyo.
Kauli hiyo ya Makamba
ameitoa leo wakati wa kufungua kongamano kubwa la siku moja la Umoja wa
Madereva wa pikipiki Mwanza lililofanyika katika uwanja wa michezo wa
Nyamagana Jijini hapa, alisema kwamba kuna baadhi ya watu wameanza
kuhoji ujio wangu Mwanza “Niko hapa kwa ajili ya shughuli hii
mliyonialika bali kuja kushiriki Kampeni muhimu ya Bima ya Afya kwa
ajili ya Usalama wa badae” na si vinginevyo.
Makamba amesema kwamba upatikanaji wa Leseni kwa urahisi na uharaka usiwe tiketi ya Kifo kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment