MTEMVU AZIDI KUWAPATIA WATANZANIA KAZI DUBAI
Mwenyekiti wa Kampuni ya Bravo, Abbas Mtemvu (kulia)
akimkabidhi Mkazi wa Bagamoyo, Asha Vitalis tiketi ya ndege na nyaraka
zingine kwa jili ya safari ya kwenda kufanya kazi Dubai, aliyotafutiwa
kazi na kampuni hiyo. Hafla hiyo ya kukabidhi tiketi kwa Watanzania
wawili walioondoka kwenda kufanya kazi Dubai, ilifanyika Dar es Salaam
juzi. Mpaka sasa kampuni hiyo imewatafutia kazi ughaibuni zaidi ya
Watanzania 100.
Mwenyekiti
wa Kampuni ya Bravo, Abbas Mtemvu (kulia) akimkabidhi Mkazi wa
Kinondoni, Neema Ndunguru tiketi ya ndege na nyaraka zingine kwa ajili
ya safari ya kwenda kufanya kazi Dubai, aliyotafutiwa na kampuni hiyo.
Hafla hiyo ya kukabidhi tiketi kwa Watanzania wawili akiwemo Asha
Vitalis (aliyekaa kushoto) walioondoka jana kwenda kufanya kazi Dubai,
ilifanyika Dar es Salaam juzi. Mpaka sasa kampuni hiyo imewatafutia kazi
ughaibuni zaidi ya Watanzania 100.
Mtemvu akiwasihi Asha na Neema kulinda maadili na heshima ya Tanzania wakiwa kazini
Asha na Neema wakisikiliza kwa makini wakati Mtemvu alipokuwa akizungumza nao kuhusu ajira yao hiyo
Mtemvu akiwa na Asha, Neema pamoja na baadhi ya wadhamini wao na baadhi ya maofisa wa Kampuni ya Bravo.
Mtemvu
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Temeke, Dar es Salaam, akiwa katika
picha ya pamoja na Asha (kushoto) na Neema baada ya kuwakabidhi tiketi.
PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
No comments:
Post a Comment