SHIRIKA LA MAENDELEO CIDA KUPITIA MRADI WA WAZAZI NA MWANA (THE MnW PROJECT) LAKABIDHI SIMU SITINI MKOANI RUKWA KURAHISISHA MAWASILIANO KATIKA VITUO VYA AFYA
Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akipokea boksi la simu
kutoka kwa Bi Safia Telatela ambae ni Mratibu wa Mradi wa Wazazi na
Mwana nchini (The WnM Project) kwa ajili ya kusaidia mawasiliano kwa
vituo vya afya Mkoani Rukwa katika kupambana na vifo vya mama wajawazito
na watoto wachanga. Jumla ya simu sitini aina ya Nokia zimetolewa
katika maeneo ya mradi huo Mkoani Rukwa ambayo ni Halmashauri ya Wilaya
ya Sumbawanga Vijijini, Kalambo na Nkasi. Akizungumza katika hafla hiyo
Katibu Tawala Mkoa hu amelishukuru shirika la maendeleo CIDA kwa
kufadhili mradi huo utakaosaidia kuokoa maisha ya mama wajawazito na
watoto kwa kurahisisha mawasiliano na sehemu zenye huduma sahihi za
afya.
Afisa
Tawala wa Mradi huo wa Wazazi na Mwana (MnW) Bwana Mashauri Ndebile
akionyesha moja ya simu hizo aina ya Nokia kwa waandishi wa habari
waliohudhuria katika hafla hiyo ya makabidhiano. Mradi huo unafadhiliwa
na Shirika la Maendeleo CIDA na kutekelezwa na Miradi Mitatu ya Plan,
Africare, Jhpiego kwa kushirikiana na MOHSW. Mradi huo unatekelezwa
katika Mikoa miwili nchini ambayo ni Mwanza kwa Wilaya za Ilemela na
Sengerema na Rukwa kwa Wilaya za Kalambo, Nkasi na Halmashauri ya Wilaya
ya Sumbawanga Vijijini.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akizindua simu hizo kwa kupiga simu moja ya majaribio.
Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima (kushoto) akimkabidhi
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Ndugu Kimulika Galikunga
Boksi moja lenye simu ishirini kwa ajili ya vituo vya afya katika
halmashauri hiyo.
Bi
Safia Telatela ambae ni Mratibu wa Mradi wa Wazazi na Mwana nchini (The
WnM Project) akizungumza katika hafla hiyo ambapo alisema lengo kubwa
la mradi huo ni kuona vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga
vinapungua na hatimae kuisha kabisa, alisema hilo litawezekana pale
jamii, taasisi binafsi, mashirika ya maendeleo na Serikali
zitakaposhirikiana katika kuleta ustawi katika eneo hilo.
Picha ya Pamoja(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)






No comments:
Post a Comment