Header Ads

LOWASA ANUSURIKA KUFA KATIKA AJALI YA NDEGE ILIYOTEKEA ARUSHA LEO.


Mhe. Edward Lowassa.
Abiria kadhaa akiwemo aliyekua Waziri Mkuu na Mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa leo December 13 wamenusurika kifo, baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kupasuka matairi yote manne ya nyuma wakati ilipokuwa ikitua katika uwanja wa ndege wa Arusha mchana mchana huu.
Image
Pichani ni ndege aliyopata nayo ajali Lowasa baada ya kupasuka magurudumu yake  manne ya nyuma.
Ndege hiyo ni mali ya shirika la ndege la Precision aina ya ATR ilipata ajali hiyo wakati ikitua Arusha.ambapo Matairi yote manne ya nyuma yalipasuka na kusababisha taharuki kubwa kwa abiria, Jumla ya watu 41 waliokua kwenye ndege hiyo, ikiwa ni abiria 39 na wafanyakazi 4 wametoka salama

No comments:

Powered by Blogger.