MBUNGE FILIKUNJOMBE ATIMIZA AHADI ZAKE KWA KANISA LA ANGLIKANA ILELA LUDEWA
![]() |
| Waumini wa Kanisa la Anglikana Ilela Ludewa wakimshangilia mbunge wao Deo Filikunjombe wakati akitolea ufafanuzi wa misaada anayoitoa kanisani hapo ,wakati wa ibada ya Krismas |
![]() |
| Mmoja kati ya waumini wa kanisa hilo akishukuru kwa kulala chini wakati mbunge wao akitoa misada yake |
![]() |
| Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe wa pili kulia akikabidhi msaada wa marumaru seti 100 kwa mchungaji wa kanisa la Anglikana mtaa wa Ilele Ludewa mchungaji Canon Ngoye |
![]() |
| Wananchi na waumini wa kanisa la Anglikana mtaa wa Ilela Ludewa wakimuwekea mikono ya baraka mbunge Deo Filikujombe baada ya kukabidhi misaada kanisan i hapo |
![]() |
| Waumini wa kanisa la Anglikana mtaa wa Ilela Ludewa akifurahi pamoja na mke wa mbunge Deo Filikunjombe Bi Habiba Filikujombe mwenye nguo nyekundu kati |
![]() |
| Waumini wa kanisa hilo wakimshangilia mbunge wao |
![]() |
| Mmoja kati ya waumini wa kanisa hilo akimfuta jasho mbunge Deo Filikunjombe kama ahsante kwa kuwajali wapiga kura wake |
![]() |
| Mbunge Filikunjombe akitoa neno kwa wapiga kura wake kanisani hapo |
![]() |
| Mbunge Deo Filikunjombe akitoa neno |
![]() |
| Mkuu wa wilaya ya Ludewa Juma Madaha kulia akiwa na mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kati na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa Bw Kolimba wakati wa ibada ya Krismas jana |
Mchungaji wa kanisa la Anglikana mtaa wa Ilela Canon Ngoye akikabidhiwa kinada na mbunge Deo Filikunjombe
Mchungaji Ngoye akikabidhiwa saruji mifuko 20 kutoka kwa mbunge Deo Filikunjombe wakati wa ibada ya Krismas
..........................................................................................................................................
MBUNGE wa jimbo la Ludewa mkoani
Njombe Deo Filikunjombe amekabidhi msaada wa vitu mbali mbali
kwa uongozi wa kanisa la Angilikana mtaa wa Ilela wilaya ya
Ludewa kama sehemu ya kutimiza ahadi yake kwa waumini wa
kanisa hilo.
Mbunge huyo alitimiza ahadi hiyo
wakati wa idaba ya Krismas ambapo alijumuika na familia yake
kusali pamoja na kula na wagonjwa wa kituo cha afya Manda kama
sehemu ya mwendelezo wa ushirikiano wake na wapiga kura wake .
Alisema kuwa kila sikukuu amekuwa
na utamaduni wa kuzunguka katika moja kati ya kanisa la jimboni
kwake na kula sikuku ya wagonjwa pamoja na kusali na waumini wa
madhehebu mbali mbali jimboni humo lengo likiwa ni kuhimiza
shughuli za maendeleo jimboni .
Hata hivyo akizungumzia mambo mbali
mbali ya kimaendeleo katika jimbo hilo alisema kuwa ameendelea
kuisukuma serikali kutatua kero za wananchi wa jimbo la Ludewa
ikiwa ni pamoja na kuboresha miundo mbinu ikiwemo barabara , afya
,elimu ,maji na kero nyingine ambazo wananchi wamekuwa wakihitahi
ufumbuzi wake.
Filikunjombe alisema kuwa kuhusu
kilichotokea bungeni kwa mawaziri wanne kuenguliwa uteuzi wao
yeye kama mbunge anaona walichokipata mawaziri hao ni haki yao na
kamwe hataacha kuwapigania wananchi wake wa Ludewa kwa kuwanyoshea
vidole mawaziri wasiowajibika katika nafasi zao.
Kwani alisema mbali ya mawaziri hao
bado wapo viongozi mbali mbali wa serikali ambao wamekuwa
wakifanya kazi kimazoea kwa kushindwa kuwajibika katika nafasi zao
na kusababisha kero kwa wananchi na hata kuichukia serikali yao
iliyopo madarakani.
Pia alimpongeza Rais Dr Jakaya
Kikwete kwa kutimiza kwa wakati ahadi yake ya gari la wagonjwa
katika Hospital ya wilaya ya Ludewa ahadi ambayo aliitoa wakati wa
ziara yake mkoani Njombe mapema mwaka huu.
Kwani alisema kuwa utekelezaji wa
ahadi za Rais kwa wananchi wa jimbo la Ludewa zinaendelea
kuwavutia wananchi wa jimbo hilo na kuwataka wananchi wa
Ludewa kuwa wavimilivu na kuendelea kuwa na imani na viongozi
wao na kuacha kulalamika pale ahadi husika inapochelewa kutolewa
.
Miongoni wa misaada iliyotolewa
na mbunge huyo ni pamoja na marumaru seti 100, mifuko 20 ya
saruji ,kinada cha kisasa kwa ajili ya kanisa na sare seti mbili
za kwaya kanisani hapo.













No comments:
Post a Comment