Wilaya ya Kaskazini B watakiwa kutumia fursa za ajira kiwanda cha sukari Mahonda
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi
akitoa salamu kwenye mkutano wa hadhara wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja
uliofanyika kwenye kiwanja cha michezo cha Mkaratini kilichopo ndani ya
Jimbo lake la Kitope.
Baadhi
ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakifuatilia matukio yaliyokuwepo
kwenye Mkutano wa Hadhara wa Wana CCM wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Hapo
Kitope ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo Haji
Juma Haji.
Wana CCM walijikuta
wakinengua wakati Kikundi cha burudani cha CCM Big Star kikifanya vitu
vyake kwenye mkutano wa hadhara wa CCM mkoa wa Kaskazini Unguja
uliofanyika kwenye kiwanja cha michezo cha Mkaratini kilichopo ndani ya
Jimbo lake la Kitope.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Ombi hilo limetolewa
na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akitoa
salamu maalum kwenye Mkutano wa hadhara wa Wanachama wa Chama cha
Mapinduzi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika katika uwanja wa
michezo wa Mkaratini ndani ya Jimbo lake la Kitope.
Na Othman Khamis Ame, OMPR
Wananchi wa Majimbo ya
Donge, Kitope na Bumbwini yaliyomo ndani ya Wilaya ya Kaskazini “B”
wameombwa kuitumia fursa na bahati waliyoipata ya uwepo wa kiwanda cha
Sukari Mahonda ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa nafasi
za ajira wakati kitakapoanza rasmi kazi zake za uzalishaji wa sukari.
Balozi Seif alisema
tabia ya baadhi ya watu kujaribu kufanya hujuma kwa kuchoma moto
mashamba yaliyooteshwa miwa ya kiwanda hicho inaweza kuwafukuzisha
wawekezaji ambao tayari wameshaonyesha nia ya kutaka kuwekeza vitega
uchumi vyao hapa Nchini.
No comments:
Post a Comment