UVCCM kutumia Milioni 800/- ujenzi wa jengo jipya la Ofisi kuu ya UVCCM
Mwenyekiti
wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Mh. Sadifa Juma Khamis akitoa Taarifa
fupi kwenye Mkutano wa kutambulishana baadhi ya wajumbe wa Kamati ndogo
ya kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa Jengo Jipya la Ofisi Kuu ya
UVCCM Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kamati
ndogo ya kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa Jengo Jipya la Ofisi Kuu
ya UVCCM Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, kulia Yake Makamu Mwenyekiti wa
Kamati Hiyo waziri Mkuu Mstaafu wa SMT Mh. Edward Lowasa pamoja na
wajumbe wengine wakiwa katika mkutano wa mwanzo wa Kamati hiyo.
Mkutano huo uliofanyika kwenye Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi iliyopo Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es salaam.
Picha Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Na Othman Khamis Ame, OMPR
Zaidi ya shilingi
Milioni Mia Nne na Nne { 204,409,440/- } zinatazamiwa kutumika katika
ujenzi wa jengo jipya litakalokuwa na vitega uchumi la Ofisi Kuu ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi uliopo hapo katika eneo la Ghimkhana Mjini Zanzibar.
Hayo yamejiri wakati wa Mkutano maalum
wa kujitambulisha uliofanyika Ofisi ndogo ya Makamo Makuu ya CCM
Iliyopo Mtaa wa Lumumba Mjini Dar es salaam kufuatia kikao cha Baraza
Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM kilichokutana Mwezi wa sita mwaka huu na
kufikia maamuzi ya kuunda
Kamati ndogo kwa ajili ya kutafuta fedha za ujenzi wa Ofisi hiyo.
Wajumbe wa Kikao hicho
walimpendekeza Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM
ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo na Makamu Mwenyekiti wake ni Waziri Mkuu
Mstaafu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Edward
Lowasa.
Akitoa Taarifa fupi
kwenye Mkutano huo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Mh. Sadifa
Juma Khamis alisema Uongozi wa Baraza Kuu la Umoja hupo umefikia hatua
hiyo katika azma yake ya kuona Umoja huo unajiendesha kiuchumi na
kuepuka mpango wa utegemezi.
No comments:
Post a Comment