Header Ads

Balozi Seif akagua miradi ya Serikali


 Mshauri wa mambo ya Ufundi wa Mamlaka ya Uwanja wa  Ndege Nd. Fredrick Nkya akimuonyesha ramani ya ujenzi wa uwanja wandege wa Zanzibar  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika kiwanjani hapo kukagua shughuli za 

Wahandisi wa Kampuni ya Sogea Satom ya Ufaransa  wakiendelea na haraki zao za ujenzi wa njia za kurukia na kutulia ndege katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume uliopo Kiembna Samaki.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiuagiza Uongozi wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege wa Zanbzibar kuiandikia Serikali mapungufu yalioyojichomoza katika zoezsi zima la ujenzi wa uwanja wa ndege ambalo haliko katika uwezo wao mara baada ya kutembelea ujenzi huo.
 



 Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d akimfahamisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif hatua iliyofikiwa ya matengenezo makubwa ya majengo ya Kiwanda cha Mpiga chapa Mkuu wa Serikali yaliyopo Maruhubi.Kushoto yao ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Dr. Aboud Sheikh Rajab
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Dr. Aboud Sheikh Rajab akifafanua jambo mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyefika kukagua maendeleo ya metengenezo ya majengo ya kiwanda cha Uchapaji yaliopo Maruhubi.
Kulia yao ni Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d.
 
Picha na Hassan Issa wa-OMPR – ZNZ.
  
Harakati za matengenezo na ujenzi wa njia za kupitia ndege wakati wa kuruka, sehemu ya maegesho ya ndege pamoja na ujenzi wa uzio katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume uliopo Kiembe samaki zimekuwa zikiendelea vyema.
 
Ujenzi huo unaotarajiwa kukifanya kiwanja hicho kuwa katika hadhi inayokubalika Kimataifa unafadhiliwa kwa pamoja kati ya Benki ya Dunia { World Bank } kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amefanya ziara ya kukagua Mradi huo wa ujenzi uliojumuisha kazi tatu zinazokwenda sambamba za njia za kurukia, jengo la abiria pamoja na eneo jipya la maegesho ya ndege kubwa .
 
Akitoa taarifa  fupi ya mradi huo mkubwa Mshauri wa mambo ya Ufundi wa Mamlaka ya Uwanja wa  Ndege Nd. Fredrick Nkya alieleza kwamba mradi huo unatekelezwa kwa kasi kubwa bila ya kuathiri  urukaji na utuaji wa ndege sambamba na mazingira ya uwanja wa ndege.
Nd. Fredrick alisema mradi wa ujenzi wa bara bara za kurukia na kutulia ndege pamoja na maegesho ya ndege unaofanywa na Kampuni ya Sogea Satom ya Ufaransa ulichelewa kuanza kama ulivyokusudiwa kutokana na eneo moja la kazi hiyo kuzunguushiwa uzio na kampuni iliyotangulia mwanzo kujenga jengo la abiria.
Alifahamisha  kutokana na ufinyu wa maegesho ya ndege katika maeneo yaliyopo hivi sasa yenye mraba wa mita 21,000 mkandarasi wa ujenzi huo amelazimika kujenga eneo la muda lenye mraba wa mita 8,200.

No comments:

Powered by Blogger.