TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
[DIWANI ATHUMANI - SACP] KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
“PRESS RELEASE” TAREHE 24. 11. 2013.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA MALI YA WIZI.
MNAMO
TAREHE 24.11.2013 MAJIRA YA SAA 03:30HRS HUKO ENEO LA MAFIATI KATA YA
MAANGA ,TARAFA YA IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA
DORIA WALIWAKAMATA 1. YUSTA D/O JACKSON, MIAKA 25, , MNYIHA NA 2.
ESTER D/O SIMFUKWE, MIAKA 35, KYUSA. WATUHUMIWA WOTE NI WALINZI WA
KAMPUNI YA ILONJE SECURITY COMPANY WAKAZI WA MTAA WA SANGU WALIKAMATWA
WAKIWA NA VITI 15 VYA PLASTIKI MALI YA SHULE YA SEKONDARI SANGU. MBINU
NI KUIBA VITI HIVYO SHULENI WAKATI WAKIWA KAZINI [LINDONI]. THAMANI
HALISI YA VITI HIVYO BADO KUFAHAMIKA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI
WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII
KUACHA TABIA YA KUJIPATIA KIPATO KWA NJIA ZISIZO HALALI KWA TAMAA YA
UTAJIRI WA HARAKA. AIDHA ANATOA RAI KWA WAAJIRI KUWA NA UTARATIBU WA
KUFANYA UCHUNGUZI KUWAFUATILIA HUSUSAN WALINZI WANAOWAAJIRI ILI
KUEPUKANA NA WATU WASIO WAAMINIFU.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI - SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment