MTOTO WA RAIS JAKAYA KIKWETE ACHUKIZWA NA SIASA ZA CHUKI NDANI YA CHADEMA NA KUPELEKEA MHE ZITTO KABWE NA WENZAKE KUVULIWA VYEO.
RIDHIWANI KIKWETE.
BAADHI ya watu maarufu nchini akiwemo mtoto wa Rais Kikwete, Ridhiwan Jakaya Mrisho Kikwete wamezipokea taarifa za kuvuliwa wadhifa wa unaibu Katibu Mkuu wa CHADEMA kwa Zitto Kabwe kwa mitazamo tofauti.
Zitto alivuliwa uongozi wa Naibu Katibu Mkuu Taifa na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa tuhuma za kukisaliti chama hicho.
Haya ni maoni ya Ridhiwani Kikwete aliyoiweka katika ukurasa wake wa facebook na twitter kuhusiana na sakata hilo:
Naendelea kujifunza matunda ya Siasa za Chuki na Ukanda zinavyoumiza siasa za Tanzania. Mungu anatuasa kupitia vitabu vitakatifu kuwa ” ili kuepusha balaa dogo kutokea, basi liwe balaa kubwa zaidi ya hilo.”. Imani kuwa aliloandika limetimia…
No comments:
Post a Comment