Soma Taarifa Maalum Kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani Ya Nchini:Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr Emmanuel Nchimbi,
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Kutokana na Maboresho
yanayoendelea ndani ya Jeshi la Polisi kumekuwepo na mikakati mbalimbali
inayolenga uboreshaji wa miundombinu yake, ikiwa ni pamoja na kupata
ofisi, vituo vya polisi, makazi ya kuishi askari makambini, vifaa na
vitendea kazi ili kuimarisha ulinzi na usalama nchini.Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi iliona kuna umuhimu wa
kuanzisha Shirika la uzalishaji mali la Polisi (Tanzania Police Corporation
Sole) ili kuendelea kufanikisha malengo ya maboresho yanayoendelea.
Kufuatia hatua hiyo
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliridhia kuanzishwa
kwa Shirika la Uzalishaji ndani ya Jeshi la Polisi baada ya kusaini
Amri ya uanzishwaji Shirika hilo tarehe 27/9/2012 kwa mujibu wa sheria
ya mwaka 1974 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2000.
Mara baada ya
kusainiwa na Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, kwa mujibu wa sheria ameteua Bodi ya Shirika hili na kumteua
Ndugu EMMANUEL HUMBA kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo kwa miaka mitatu kuanzia
tarehe 19/9/2013, aidha amewateua wajumbe wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi
hiyo:-
(2)Jehad Abdallah
Jehad –Msajili Bodi ya Wakadiriaji na Wasanifu
Majengo
(3) Melkior Temu-
Mipango, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
(4) T.M.E Andengenye
–DCP Mkuu wa Utawala Jeshini
(5) A. Nyamhanga
–ACP-Mkuu wa Kitengo cha Mipango na Bajeti Jeshi la
Polisi
(6)Samwel Marco-Meneja
Hazina –(Tressure)-TIB
(7) John Mathew-
Kaimu Mkurugenzi Mhamasishaji- TIC
Katika uteuzi huo amemteua
pia DCP- SOSPETER M. KONDELA kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kwanza wa Shirika
hilo.uteuzi huo unaanza mara moja.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI,
18 NOVEMBA, 2013.
No comments:
Post a Comment