Mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro akisoma somo kwenye biblia wakati wa ibada maalumu ya shukrani kwenye Kanisa la (KKKT ) Usharika wa Kibamba nje kidogo ya Jiji la Dare Salaam jana
Mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro akisoma
somo kwenye biblia wakati wa ibada maalumu ya shukrani kwenye Kanisa la
(KKKT ) Usharika wa Kibamba nje kidogo ya Jiji la Dare Salaam jana.
Picha na Sanjito Msafiri.
--
Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro ambaye
alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na mzazi mwenzake, Anthery Mushi,
amefanya ibada na kusema: “Namshukuru Mungu kwa kumponya.”
Ni mara ya kwanza Saro kuzungumza tukio hilo tangu
aliporuhusiwa kutoka Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu, MOI ya
Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa.
Katika ibada hiyo iliyofanyika katika Kanisa la
Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Kibamba, Jimbo la Magharibi, Ufoo
huku akitokwa na machozi na wakati mwingine kushindwa kuzungumza
alisema: “Ni miujiza tu ya Mungu yeye kunifanya mimi kuwa hai leo.”Kwa habari zaidi Bofya na Endelea........
No comments:
Post a Comment