Kutoka Gazeti la Mwananchi Leo:Bunge lakataa kubariki ‘Division 5’
Mwenyekiti Wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii Magreth Sitta
----
Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, imevikataa viwango vipya
vya alama za ufaulu kwa elimu ya sekondari vilivyotarajiwa kuanza
kutumika mwaka huu na kutaka utaratibu na alama zilizotumika mwaka jana,
zitumike kupanga matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne wa mwaka
huu.
Serikali ilitangaza utaratibu mpya wa alama za
Mitihani ya Kidato cha Nne na Sita kwa kufuta Daraja la Sifuri na kuleta
Daraja la Tano.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Stephen
Ngonyani alisema jana kuwa kamati hiyo ilichukua uamuzi huo kwa kuwa
pamoja na udhaifu ulio kwenye alama hizo, kamati yao haikuhusishwa
katika mchakato wa kuandaa alama hizo.
“Mwenyekiti wangu (Margaret Sitta) alisema kile
hakiwezekani, kuna viwango ambavyo wameleta havipo kwenye nchi nyingine
duniani, tumewaambia wakavifanyie kazi walete tena,” alisema mbunge huyo
wa Korogwe Vijijini, ambaye ni maarufu zaidi kwa jina la Profesa Maji
Marefu.Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea.........
No comments:
Post a Comment