ILO YAENDESHA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI NA KUJIKINGA NA VVU KWA WANAWAKE CHALINZE
Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi ILO
Getrude Sima (kushoto) akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi
Kaimu Afisa Tarafa ya Chalinze kata ya Pera Bw. Rashid Kiwamba (kulia)
kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya siku sita kuhusu maambukizi
ya Virusi vya Ukimwi kwa Wanawake wasiokuwa kwenye ajira rasmi na
wanaoishi pembezoni katika juhudi za kudhibiti maambukizi mapya ya
Virusi vya Ukimwi.
-
.Zaidi ya wanawake 220 wafikiwa na mradi huo wa Shirika la Kazi Duniani
Na Damas Makangale, Chalinze Moblog
SHIRIKA LA KAZI DUNIANI (ILO)
limeendesha mafunzo ya siku sita kuhusu maambukizi ya Virusi vya Ukimwi
kwa Wanawake wasiokuwa kwenye ajira rasmi na wanaoishi pembezoni katika
juhudi za kudhibiti maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi. Moblog
inaripoti.
Mradi huo wa Shirika la Kazi Duniani
(ILO) unalenga wanawake wote ambao wapo pembezoni wa barabara na
mipakani kwa sababu wapo katika hali ya hatarishi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoa
Pwani Wilayani Chalinze, Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi kutoka
Shirika la Kazi Duniani (ILO) Getrude Sima amesema ndani ya siku sita
mradi wa mapambano ya Ukimwi chini ya ILO umewafikia wanawake 120 katika
kata za Pera, Chamakweza, Mpingo, Bwilingu, Msolwa na Mdaula.
Mshauri wa Biashara wa shirika
lisilokuwa la Kiserikali (NGO) TAPBDS Bi. Theresia Kato akifundisha
wakinamama wa Chalinze (hawapo pichani) jinsi ya kuandika na kuandaa
mchanganuo wa biashara katika mafunzo hayo ya siku sita yaliyoandaliwa
na Shirika la kazi Duniani (ILO).
Amesema tangu mradi uanze kutekelezwa
hapa nchini wakutoa mafunzo ya ujasiriamali na kujikinga na Virusi vya
Ukimwi wameweza kuwafikia wanawake 220 nchi nzima katika maeneo ya
pembezoni na mpakani kama vile Tunduma, Kyela na Namanga.
“Unajua wanawake wengi wanakuwa katika
kundi hatarishi pale wanapokuwa katika maeneo ya mpakani na pembezoni
mwa barabara kwa mfano Chalinze kwa sababu ya muingiliano wa watu hasa
Madereva na Wafanyabiashara,” amesema Sima.
Sima ameongeza kuwa katika mradi huu wa
mapambano ya Ukimwi malengo ni kumuelimisha Mwanamke ili ajitambue na
aweze kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa kumfundisha stadi
za maisha pamoja na ujasiriamali.
Amesema mradi unalenga wanawake
wasiokuwa katik ajira rasmi ili kuongeza muamuko miongoni mwa wakinamama
mitaani na vijijini ili waweze kukabiliana na vishawishi katika sehemu
zao wanazoishi.
Bi. Theresia Kato akiwaelekeza washiriki namna ya kujaza fomu za kuombea mikopo kwa taasisi mbalimbali.
Kwa upande Mshauri wa Biashara toka
shirika lisilo kuwa la Kiserikali TAPBDS, Theresia Kato amesema kuwa
biashara ndogo ndogo ni muhimu katika kumjengea mwanamke uwezo wa
kujiamini na kujitegemea.
“lazima wanawake waamuke ili waweze
kuanzisha biashara zao na kuandika mchanganuo wa biashara na kutafuta
mitaji kupitia taasisi mbalimbali za fedha hapa nchini,” amesema.
Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi ILO
Bi. Getrude Sima akisisitiza jambo kwa washiriki kuhusiana na mafunzo
waliyoyapata yakawe chachu ya kuleta maendeleo.
Picha juu na chini ni baadhi ya wakinamama wa Chalinze wakifuatilia mafunzo hayo yaliyomalizika mwishoni mwa wiki.
Mgeni rasmi Kaimu Afisa Tarafa ya
Chalinze kata ya Pera Bw. Rashid Kiwamba akikabidhi vyeti kwa mmoja wa
wahitimu wa mafunzo hayo.
Mwanamke wa Kimasai Paspen Kisota akipokea cheti chake baada ya kuhitimu mafunzo hayo.
Picha juu na chini mgeni rasmi Kaimu
Afisa Tarafa ya Chalinze kata ya Pera Bw. Rashid Kiwamba na Mratibu
Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi ILO Getrude Sima wakiwa kwenye picha ya
pamoja na wahitimu.
Fundi Sanifu wa Maabara ya Afya Bw.
Rwezahura Merehiory akichukua damu kwa ajili ya vipimo vya VVU kwa mmoja
wa washiriki wa semina ya mafunzo ya Ujasiriamali na Kupambana na
maambukizi ya Virusi vya Ukimwi iliyoratibiwa na shirika la Kazi duniani
(ILO) wilaya ya Chalinze mwishoni mwa wiki.
No comments:
Post a Comment