KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI, JOHN CASMIR MINJA AMVISHA CHEO CHA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA MAGEREZA
AFISA MWINGINE ALIYEKUWA ANAHUDUMU ULINZI WA AMANI KATIKA JIMBO LA DARFUL - SUDANI LEO JIJINI DAR
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kulia) akimvisha
Cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Deus Clement
Marenge ambaye anahudumu kazi ya Ulinzi wa Amani katika Jimbo la Darful -
Sudan. Hafla ya uvalishaji cheo imefanyika leo Novemba 18, 2013 katika
Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es
Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja( kulia)
akimpongeza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Deus Clement
Marenge mara baada ya kumvisha cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Magereza leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la
Magereza, Jijini Dar es Salaam. Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Magereza, Dkt. Deus Clement Marenge ni miongoni mwa Maafisa wa Jeshi la
Magereza ambao wanahudumu kazi ya Ulinzi wa Amani katika Jimbo la
Darful - Sudan.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa nasaha
fupi mara baada ya zoezi la uvalishaji cheo kwa Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Deus Clement Marenge( hayupo pichani)
ambaye kwa sasa anahudumu kazi ya Ulinzi wa Amani katika Jimbo la Darful
- Sudan.
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakimpongeza Dkt. Deus
Clement Marenge(wa tatu kulia) kwa kutosi vinywaji kama inavyoonekna
katika picha mara baada ya hafla fupi ya uvishaji cheo kwa Afisa
Mwandamizi wa Jeshi la Magereza ambaye amevishwa cheo cha Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Magereza na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini,
John Casmir Minja(hayupo pichani).
Kamishna wa Magereza wa Huduma za Urekebishaji, Deonice
Chamulesile(aliyesimama) akimpongeza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Magereza, Dkt. Deus Clement Marenge mara baada ya zoezi la uvalishaji
cheo lililofanyika leo Novemba 18, 2013 katika Ukumbi wa Mikutano wa
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.Picha zote na
Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza
No comments:
Post a Comment