Serikali yatoa ufafanuzi wa vifaa vya kutoa risiti za kieletroniki.
Naibu Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kulia)akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu utata wa vifaa vya kieletronik vya kutoa risiti(EFD) |
======== ======= ========
Na Magreth Kinabo
Serikali
imesema imeshaelekeza wasambazaji wa vifaa vya eletroniki vya kutoa
risiti (EFD) kuuzwa kwa bei tofauti kulingana na ubora wake.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum
wakati akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa
Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri huyo ,alitoa ufafanuzi huo baada kuulizwa swali na waandishi wa
habari kufutia mgomo wa wafanyabiashara unaoendelea katika baadhi ya
mikoa kufutia kifaa hicho kuuzwa kwa bei ya Sh. 700,000 na 800,000
ambayo wanadai ghali.
“ Utumiaji wa EFD si kumkomoa mfanyabiashara bali ni kuongeza mapato ya Serikali katika kuendeleza maendeleo ya nchi".
Kwa
mujibu wa Naibu Waziri huyo alisema vifaa hivyo vipo vinavyouzwa
kuanzia bei ya 100,000 na kuendelea,hivyo na kuwataka wasambazaji kuuza
vifaa hivyo kulingana na bei iliyopangwa kulingana na ubora.
No comments:
Post a Comment