Mkutano wa wadau wa Bima ya Afya wafanyika Chake Pemba
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba , Meja Mstaafu, Juma Kassim Tindwa, akifunguwa mkutano wa Wadau wa Bima ya Afya NHIF, huko katika Hoteli ya Hifadhi Pemba.
.
Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya , Ali
Othman, akizungunza jambo lwa Wadau wa Mfuko huo huko katika Hoteli ya
Hifadhi Chake Chake Pemba , katika maadhimisho ya siku ya wadau .
Mwandishi mwandamizi wa ZBC TV- Pemba, Nasra Moh'd Khatib, akichangia mada katika mkutano wa Wadau wa Bima yaTaifa ya Afya , huko hoteli ya Hifadhi Chake Chake Pemba , juu ya Humduma ya Uzazi kwa Wanachama wa Mfuko huoPICHA NA BAKAR MUSSA-PEMBA.
Marekani yaipatia Zanzibar Dola Laki mbili kusaidia Sekta ya Kilimo nchini
Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Zanzibar Affan Othman akizungumza
na Ujumbe kutoka Marekani kabla ya kutiwa Saini Msaada wa Ruzuku ya Dola
za Kimarekani Laki 2 kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo USAID
ili kuinua kipato cha Wakulima Wadogowadogo wa Zanzibar .
Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Zanzibar Affan Othman kulia na
Mwenzake kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Marekani USAID Tom
Hobgood wakitiliana saini ya Msaada wa Ruzuku ya Dola za Kimarekani Laki
2 kwa lengo la kuinua kipato cha Wakulima Wadogowadogo wa Zanzibar.
Mkufunzi wa Mradi wa Feed the Future kutoka Marekani Mr. Martin akizungumza na baadhi ya Wakulima wa Bonde la Mpunga la Kipange, Donge Kaskazini Unguja ambao walipatiwa Mafunzo ya kilimo cha kisasa kupitia Mradi huo.
Wakulima wa Bonde la
Mpunga la Kipange wakimsikiliza Mkufunzi wa Mradi wa Feed the Future
kutoka Marekani Mr. Martin hayupo pichani alipofika kuangalia maendeleo
yao katika shamba la majaribio kipange.
(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Serikali
ya Marekani kupitia Shirika lake la Kimataifa la Maendeleo la USAID
imeisaidia Wizara ya Kilimo na Maliasili Zanzibar Ruzuku ya jumla ya
Dola za Kimarekani Laki mbili ili kusaidia maendeleo ya Sekta ya Kilimo
nchini.
Msaada
huo ni mwendelezo wa Juhudi ya Serikali ya Marekani katika kuongeza
uzalishaji na kipato cha wakulima wadogo wadogo wa Zanzibar kupitia
Mradi wao ujulikano kama "Lisha Kizazi Kijacho"
Akitoa
Salamu zake kabla ya kusaini Msaada huo kiongozi wa Mradi huo kutoka
Marekani Tom Hobgood amesema wameamua kuendelea kuisaidia Zanzibar
kutokana na misaada yao kutumika vizuri na kufikia lengo lililokusudiwa.
Amesema
juhudi zilizochukuliwa na Wizara ya Kilimo za kuwajengea uwezo wakulima
wadogowadogo zimezaa matunda na hivyo Wakulima waliopewa mafunzo kupitia
mradi wa "Lisha Kizazi Kijacho" wamebainisha faida walizozipata ikiwa
ni pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wao.
Tom
ameongeza kuwa Juhudi wanazozifanya kuwasadia Wakulima wa Zanzibar na
Tanzania kwa ujumla ni utekelezaji wa ahadi za Rais Obama aliyotoa
wakati wa Ziara yake Afrika mwanzoni mwa mwaka huu ambapo alibainisha
kuwa maendeleo ya Sekta ya kilimo ndio suluhu ya kuondoa Umasikini
Afrika.
Amefahamisha
kuwa Msaada huo Utanufaisha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar na
Chuo cha Kilimo Kizimbani ili kuweza kupanga utaratibu mzuri wa kilimo
cha kisasa kinachozingatia maendeleo ya Sayansi na teknolojia.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili Affan Othman
Said ameishukuru Serikali ya Marekani kwa juhudi zake za kuisaidia
Zanzibar hasa katika kuwakomboa Wananchi wa kipato cha chini.
Amesema
Kwa muda mrefu wananchi wa Zanzibar wamekuwa wakilima bila kuzingatia
taratibu zinazoendana nawakati na kwamba Msaada huo unaweza kuwa
Mkombozi wa Wakulima.
Amesema
kupitia Mradi wa "Lisha Kizazi Kijacho" wananchi wamenufaika sana kwa
kupata mafunzo ya kutayarisha Vizuri Mashamba yao na kujua Mbegu bora
kulingana na eneo husika na hivyo juhudi hizo zinafaa kuendelezwa.
Kupitia
Mradi huo Wakulima walijengewa uwezo mzuri wa kutayarisha Mashamba yao
vyema na kujua mbegu sahihi kulingana na eneo husika ili kuongeza
uzalishaji wao na kuepukana na umasikini.
Akizungumza
na Ujumbe wa Marekani Mmoja wa Wakulima waliopatiwa Mafunzo kupitia
Mradi wa"Lisha Kizazi Kijacho" Shadhil Hamis amesema Mradi huo
umewasaidia sana na kwao umekuwa kama Mkombozi dhidi ya Umasikini.
'"Kwa
kweli zamani tulikuwa hatulimi tunajiumiza tu lakini kupitia Mradi huu
ndio tunaona faida ya kilimo maana tunatumia mbegu kidogo wakati wa
kupanda lakini tunavuna mavuno ya hali ya juu kabisa" Alisema Shadil.
Ameomgeza
kuwa kabla ya kupewa mafunzo ilikuwa wanatumia Karibu Kilo 50 za mbegu
kutayarisha Shamba la Nusu Eka lakini kwa Sasa wanatumia kilo mbili
kasoro na mavuno ni mengi kuliko hata mwanzo.
Kwa
upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Juma Ali Juma amesema Mradi
huo utawawezesha kuandaa Mashamba 40 Unguja na Pemba ambayo yatatumika
kuwajengea uwezo Wakulima ili kuinua kipato chao.
Aidha
amewaomba Wakulima waliopata mafunzo kuendelea kuyatumia katika shughuli
zao na kuwaelekeza Wakulima wenzao ili hatimae Zanzibar iweze
kujikwamua na umasikini.
Awali
Mradi wa "Lisha Kizazi Kijacho" ulio chini ya Shirika la Kimataifa la
Maendeleo la Marekani USAID ulikuwa unahudumia Vituo vitatu lakini
kutokana na Msaada uliotolewa kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar utawezesha kuhudumia Mashamba 40 ambapo Jumla ya Wakulima 5600
watapatiwa Mafunzo ya kilimo cha kisasa.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment