MILLEN HAPPINESS MAGESE ATEMBELEA MAENDELEO YA MIRADI MTWARA
Mwanamitindo
wa kimataifa wa Tanzania, Millen Happiness Magese amewataka watu
binafsi na makampuni mbalimbali kujitokeza kwa wingi katika kusaidia
tasnia ya elimu hasa katika maeneo yasiyopewa kipaumbele ili kuwaokoa
watoto wa maeneo hayo kutotumbukia katika vitendo visivyo vya kimaadili.
Rai hiyo ameitoa wakati alipotembelea miradi yake aliyoifadhili ya
ujenzi wa vyumba vya madarasa na utengenezaji wa madawati.
Millen Happiness Magese akiwa amepozi na wanafunzi huku wakiwa wamekalia madawati aliyochangia katika shule hiyo.
Sehemu ya madawati yaliyotolewa na mrembo huyo katika shule ya Msingi Mjimwema.
Ujenzi
wa madarsa unaendelea katika shule ya msingi Mjimwema iliyopo manispaa
ya Mtwara ambapo mradi wa kutengeneza madawati ulikabidhiwa kwa vikundi
mbalimbali vya wajasiriamali mkoani hapo kwa mpango maalum kupitia ofisi
ya mkuu wa Wilaya, Mheshimiwa Wilman Ndile. Jumla ya madawati hamsini
na tano (55) yenye thamani ya shilingi milioni tano yalikuwa tayari
yameshatengenezwa kama walivyoahidi wajasiriamali hao wakati
wakikabidhiwa kazi ya utengenezaji wa madawati hayo.
Millen
akiwa pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mjimwema iliyopo manispaa
ya Mtwara ambapo madarasa yanajengwa na pia pia aliwanunulia wanafunzi
hao madaftari kama waonekanavyo pichani.
Madawati hayo yalikabidhiwa rasmi na Millen yalikabidhiwa kwa wanafunzi wa shule ya msingi Lilungu. Kwa
upande wa afisa elimu wa manispaa ya Mtwara Frola Aloys amewataka wadau
wa elimu kuonesha uzalendo wa hali ya juu kwa maeneo ya Kusini mwa
Tanzania huku mkuu wa shule ya msingi Lilungu Abdul Nangomwa akielezea
changamoto zinazoendelea kuikumba sekta ya elimu katika shule za msingi
wilayani Mtwara.
Millen akipozi na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mjimwema nje ya darasa jipya linalojengwa na mrembo huyo.
Mbali
na kukabidhi madawati Millen aligtembelea ujenzi unaoendelea shule ya
msingi Mjimwema na kutoa zawadi ya madaftari napenseli kwa wanafunzi hao
ambapo mpaka sasa shule in mikondo mitatu ambayo ni kuanzia darasa la
awali mpaka darasa la pili.
Ziara
hiyo ya mrembo huyo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania mwaka 2001,
ni mwendelezo wa shughuli za kijamii anazozifanya nchini Tanzania hasa
katika kusaidia makundi yenye mahitaji maalumu na yale yasiyopewa
kipaumbele.
Mwanzoni
mwa mwaka huu Millen Magese alitoa kiasi cha shilingi milioni kumi na
tano katika kusaidia huduma hiyo ya elimu katika manispaa ya Mtwara.
No comments:
Post a Comment