Rose Muhando atajwa kutumbuiza Tamasha la Krismasi
MKALI
wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando, ni miongoni mwa Watanzania
watakaotumbuiza Tamasha la Krismasi Desemba 25 mwaka huu Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Msanii
huyo anayetamba na albamu zake mbalimbali ikiwemo ya Utamu wa Yesu, pia
atatumbuiza Desemba 26 mwaka huu kwenye Tamasha la Krismasi
litakalofanyika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Krismas, Alex Msama alisema jana
kuwa hatua ya kamati yake kumalizana na Muhando imewapa faraja kubwa,
kwani huyo ni miongoni mwa waimbaji ambao Watanzania wanawapenda.
“Mungu
ni mwema, kila tunalolipanga anatusaidia sana, karibu waimbaji wote
ambao mashabiki wanawapenda, wamekuwa na ushirikiano mkubwa na sisi.
Hawana matatizo na si watu wenye tamaa, bali wanaweka mbele kutoa
huduma.
“Tayari
hivi sasa waimbaji watatu wa Tanzania tumeshakubaliana nao ambao ni
Upendo Nkone, Upendo Kilahiro na huyo Rose Muhando, kwa nje
tumeshamalizana na Ephraim Sekeleti. Bado tunaendelea na mazungumzo na
wasanii wengine wa ndani ya Tanzania na nje ya nchi ili wote waje
kutumbuiza,” alisema Msama.
Albamu
ya Utamu wa Yesu ya Rose Muhando inabeba nyimbo saba ambazo ni Utamu wa
Yesu, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu
na Achia.
Mbali
na Utamu wa Yesu, Rose Muhando pia amewahi kutamba na albamu za Uwe
Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi) na Jipange Sawasawa.
Pia amepata kung’ara katika wimbo wa Vua Kiatu, alioshirikiana na
Anastazia Mukabwa wa Kenya katika albamu ya Vua Kiatu, ambayo ilikuwa na
nyimbo kama Vua Kiatu, Ee Mungu, Usiwe Manamba, Nzizilela, Nishike
Mkono Bwana, Wanaokudharau na Mfalme.
No comments:
Post a Comment