Header Ads

KINANA NA UJUMBE WAKE WAWASILI WILAYANI KYELA MKOANI MBEYA,TAYARI KWA ZIARA YA SIKU 11


Sekretarieti kuu ya CCM,ikiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (pichani kati),Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asharose Migiro (kulia) pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye wakiwapungia wakazi mbalimbali waliofika kuwalaki mapema leo walipokuwa wakiwasili kwenye Bandari mpya ya Kiwila Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, kwa ziara ya kikazi,wakitokea wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma kwa meli. 
 Pichani shoto ni Nahodha Mkuu wa Meli ya Mv Songea akitoa maelezo mafupi namna ya moja ya chombo cha meli kinavyofanya wakati ikisafiri majini, kwa Sekretarieti kuu ya CCM,ikiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC,siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asharose Migiro pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye mapema leo walipokuwa wakienda Wilayani Kyela Mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi,wakitokea wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma kwa meli.Pichani kulia ni Nahodha msaidizi wa Meli ya Mv Songea.Conrad Shauritanga akiongoza meli hiyo.
Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asharose Migiro akiuliza jambo kwa Manahodha wa meli hiyo wakati ikiwa safarini kuelekea Wilayani Kyela Mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi,wakitokea wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma kwa meli.
 Mbunge wa jimbo la Kyela na Waziri wa Uchukuzi,Dkt Harrison Mwakyembe akimlaki kwa furaha kubwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake walipowasili mapema leo  kwenye Bandari mpya ya Kiwila, Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, kwa ziara ya kikazi,wakitokea wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma kwa meli. 
Mbunge wa jimbo la Rungwe Magharibi,Mh.David Mwakyusa akimlaki  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake waliowasilia mapema leo  kwenye Bandari mpya ya Kiwila Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, kwa ziara ya kikazi,wakitokea wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma kwa meli. Pichani kati ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mbeya (CCM),Dkt Mary Mwanjelwa akishuhudia tukia hilo
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakipokelewa na Mwenyekiti Mkoa wa Mbeya,Bwa. Godfrey Zambi wakati wakishuka ndani ya meli ya Mv Songea mapema leo  kwenye Bandari mpya ya Kiwila, Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, kwa ziara ya kikazi,wakitokea wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma. 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na baadhi ya wanachama wa CCM waliofika kumlaki na ujumbe wake mara baada ya kupokelewa vyema katika  kwenye Bandari mpya ya Kiwila, Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, kwa ziara ya kikazi,wakitokea wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma. 
  Mbunge wa jimbo la Kyela na Waziri wa Uchukuzi,Dkt Harrison Mwakyembe akitoa ufafanuzi  kwa Katibu Mkuu wa  CCM,Ndugu Kinana kuhusiana na kivuko cha Tungi ambacho kwa sasa hakifanyi kazi .Kinana na ujumbe wake tayari amewasili leo kwa meli ya Mv.Songea Wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Wilayani Nyasa mkoani Ruvuma 
 Sehemu ya kivuko cha Tungi ambachao hakitumiki kwa sasa mara baada ya kujaa mchanga,kwa sasa hakitumiki tena kama kionekanavyo pichani mapema leo.
"UMOJA NI USHINDI".! Mbunge wa jimbo la Songwe Mh.Phillip Mulugo, Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mbeya (CCM),Dkt Mary Mwanjelwa Mbunge wa jimbo la Kyela na Waziri wa Uchukuzi,Dkt Harrison Mwakyembe wakiwa wameshikana mikono kwa pamoja mara baada ya kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake

No comments:

Powered by Blogger.