Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Ujumbe Wake Wamaliza Ziara katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma na kuanza safari ya kwenda Kyela ambako ataanza ziara katika mkoa wa Mbeya.
Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, asubuhi hii amemaliza ziara yake katika
wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma na kuanza safari ya kwenda Kyela ambako
ataanza ziara katika mkoa wa Mbeya. Pichani, Kinana na wajumbe wa
sekretarieri ya CCM, Nape Nnauye (Itikadi na Uenezi) na Dk. Asha-Rose
Migiro (Siasa na Uhusiano wa KIImataifa), wakiwapungia mikono wananchi
wa Nyasa, baada ya kupanda Mv Songea katika bandari ndogo ya Mbamba Bay,
kuanza safari ya kwenda Kyenla. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nyasa,
Ernest Kahindi
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na wananchi wa Mbamba Bay, Nyasa, kabla ya kupanda meli kwenda Kyela
Katibu
wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migirob
akisalimiana na Nahodha wa Mv Songea Tom Faya, katika bandari ndogo ya
Mbamba Bay, wilayani Nyasa mkoani Ruvuma kabla ya safari ya kwenada
Kyela
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Nahodha wa mv Songea,
kabla ya safari ya kwenda Kyela kutoka bandari ndogo ya Mbamba Bay,
Nyasa. Wapili kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa Oddo Mwisho
Mkurugenzi
na Mtayarishaji Mkuu wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo, ambaye ni
baadhi ya abiria walioko katika msafara wa Kinana,akipanda mv Songea.
Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipanda mv Songea. Wanaomfuata na
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho na katibu wa NEC, Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
Wananchi
na wanachama wa CCM wa Mbamba Bay, wilayani Nyasa mkoani Ruvuma,
wakisindikiza kwa boti mv Songea wakati ikiondoka bandarini
Nahodha wa ,mv Songea na Kinana wakizungumza na waandishi wa habari. Imetayarishwa na theNkoromo Blog
No comments:
Post a Comment