Salaam Za Pongezi Kutoka Kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA(Mstaafu) Ananilea Nkya Kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini-Chadema Zitto Kabwe na Dr Kitila na Chadema
Aliyekua Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Ananilea Nkya
----
Vijana Dr Kitila na Zitto.
Nimesoma matamko yenu mliyoyatoa leo.
Nakupongezeni maana mmeonyesha kwamba mnatambua ninyi ni binadamu na si malaika. Mmetuonyesha sisi wananchi kwamba ninyi ni wanasiasa wenye hofu ya Mungu. Mmetuonyesha kwamba mmeamua
kutoa maisha yenu kuwatumikia Watanzania na si kwa maslahi yenu binafsi
au maslahi ya chama chenu CHADEMA pekee, bali maslahi ya Watanzania.
Mmeandika historia mpya inayotoa mafunzo mbali mbali.
Ninachowashauri na hiki narejea nilichokiandika kwenye
uzi uliokuwa na tamko la Zitto ni kwamba muendelee kusimama imara na
chama chenu bila kinyongo chochote kutokana na yaliyotokea mkiwa na lengo moja kupigania maslahi ya umma mpana ili NCHI YETU ISHINDE. Aidha, CHADEMA kama chama makini cha siasa, muendelee kuangalia mbele kwa umakini sana muwashinde wenye
nia chafu dhidi yenu. Na ushindi wenu utatokana na nia
yenu safi kwa nchi yenu na watu wake, umoja wenu, umakini wenu, usafi wa
matendo yenu, kuheshimiana kwenu kwenu ninyi kwa ninyi kuonyana ili kurekebishana na kisha kusameheana kwenu.
Siku zote mkumbuke, thawabu yenu kuu kama wanasiasa itatokana na jinsi siasa za chama chenu zitakavyofanikisha
kuijenga Tanzania mpya isiyo na kiwango kikubwa cha rushwa kama ilivyo
sasa, isiyo na ubaguzi wa haki kama ilivyo sasa kwamba baadhi
ya viongozi hata wakituhumiwa kutenda jinai kubwa mkono wa sheria
hauwezi kuwadaka haraka la bda kwa shinikizo ili hali mwananchi wa
kawaida akiiba hata ugali anaweza kuishia jela wiki inayofuata .
Kadhalika Tanzania mpya yenye hospitali nzuri zenye vifaa, madawa na madaktari (naamini
Dr Sengondo Mvungi asingekufa kama tulikuwa na hospitali nzuri hapa
yenye vifaa na madawa madaktari wangemuwahi), shule nzuri na Tanzania
mpya isiyo na pengo kubwa la kipato kati ya vwanasiasa na watumishi wengine wa umma n.k.
Nawatia shime wote mnaopigania wananchi na Mungu awabariki sana.
By the way you kijana Samsoni Mwigamba sikusoma tamko lake yeye kasemaje?
Ananilea Nkya E-mail:ananilea_nkya@yahoo. com
No comments:
Post a Comment