KINANA ATINGA PERAMIHO SONGEA NA KUWAKEMEA VIONGOZI WANORUMBANA KWA TAMAA YA KUGOMBEA MADARAKA, MALI
Kiongozi wa kimila wa Kabila la Wangoni, Julius John (kulia)
akimkabidhi siraha za jadi Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika
mapokezi Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma. Siraha ahizo ambazo ni ngao,
fimbo, rungu na shoka ni kwa ajili ya kumpa uwezo wa kupambana na
mafisadi na wengine wote wanaoitakia nchi mambo mabaya. Katikati ni
Mbunge wa Jimbo hilo, Jenista Mhagama.
Kinana akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi wa Kimila wa Kabila la
Wangoni, Julius John (wa pili kushoto), Katibu wa Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa wa CCM, Dk. Asha Rose Migiro (kulia) pamoja na Mbunge wa Jimbo
la Peramiho, Jenista Mhagama (wa pili kulia) baada ya kukabidhiwa
siraha za jadi.
Kinana akiangalia ngoma ya asili
Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama (katikati) akishangiliwa na
wananchi baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (hayupo
pichani) kumsifia kuwa ni kiongozi bora na kumfananisha na chuma cha
Mjerumani wakati wa mkutano uliofanyika nyumbani kwa Balozi Said Issa
mjini Peramiho, mkoani Ruvuma, akiwa katika muendelezo wa ziara ya
kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa
kwa kufuata Ilani ya CCM.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto), akinywa chai na Mbunge
wa Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama (kulia) nyumbani kwa Balozi wa
Shina CCM namba 28, Said Issa (katikati) mjini Peramiho
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (kushoto) akishiriki
kupiga gita wakati bendi ya Ngomande ikitumbuiza wakati Katibu Mkuu wa
chama hicho, Abdulrahman Kinana (hayupo pichani) alipowasili mjini
Peremiho, mkoani Ruvuma. Anayecheza kulia ni Mbunge wa Jimbo la
Peramiho, Jenista Mhagama.
Kikundi cha ngoma za asili kikitumbuiza
No comments:
Post a Comment