Kinana amaliza ziara yake jimbo la Tunduru kusini,ahamia tunduru Kaskazini leo akiendelea kukagua miradi mbalimbali ya wananchi na chama kwa ujumla.
Katibu
Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na Katibu wa
NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk Asha-Rose Migiro kujenga daraja
la mto Munjapu wilayani Tunduru.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyeshwa jinsi barabara
itakavyokuwa baada ya kukamilika kwa daraja la mto Munjapu,lililopo
kijiji cha Mnemasi, Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kuimarisha
chama,kusimamia ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 katika mkoa wa Ruvuma
akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye
na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa kwenye kijiji cha
Mchoteka kwa staili ya aina yake ya kukimbia mchaka mchaka mpaka kwenye
miradi ya ujenzi wa madarasa,maabara na nyumba za walimu katika shule ya
Sekondari ya Mchoteka wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa moja ya
nyumba za walimu wa shule ya Sekondari Mchoteka,wilayani Tunduru.
Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akishiriki
uchimbaji wa msingi wa vyumba vya maabara ya shule ya sekondari Mchoteka
wilayani Tunduru.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na umati wa wananchi
wa kijiji cha Mchoteka wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha
Mchoteka waliofurika kutaka kumsikiliza, Katibu Mkuu alikuwa na ratiba
ya kuonana na kumsalimia balozi wa nyumba kumi lakini kwa namna wananchi
walivyojaa ilibidi ahutubie wananchi kwanza kabla ya kuonana na Balozi
wa nyumba kumi.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa KImataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Mchoteka wilayani Tunduru.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wananchi wa kijiji
cha Mchoteka waliojitokeza kwa wingi kuja kuwapokea viongozi wao wa
kitaifa.
Babu
Akuilaya (Babu Mkuu) kama heshima aliyopewa na Machifu wa Mchoteka,Ndugu
Abdulrahman Kinana akiongea na wananchi wa kijiji cha Mchoteka na
kuwashukuru kwa heshima waliyompa.
Katibu
Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi kwa
wanachama wapya wa CCM ambapo zaidi ya wanachama 100 wamejiunga na CCM
katika kata ya Mchoteka.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata mapokezi mazuri wakati
akiwasili katika kata ya Nalasi,kijiji cha Nalasi wilaya ya Tunduru.
Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiimba na
akina mama wakazi wa kata ya Nalasi waliojitokeza kwa wingi kuupokea
ugeni .
Umati
wa wakazi wa Kijiji cha Nalasi ukiwa umejaa kumsikiliza Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara katika mkoa wa
Ruvuma.
No comments:
Post a Comment