Header Ads

FRANK MTAO M/KITI MPYA NSW AUSTRALIA

Mmmiliki wa kampuni ya 2 Eyez Production na aliyewahi kuwa mtangazaji wa kituo cha television cha channel ten Bw. Frank Mtao, jumamosi iliyopita ya tarehe 23/11/13 alifanikiwa kunyakua kiti cha uenyekiti wa chama cha jumuiya ya watanzania waishio New South Wales nchini Australia.

Katika kinyang'anyiro hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Lethington uliopo kitongoji cha Summer Hill, mjini Sydney, Frank alifanikiwa kumshinda mpinzani wake ambaye ni mkazi wa muda mrefu katika jiji la Sydney Bw Christopher Banda kwa kura 55 dhidi ya 6 alizozipata Chriss.

Baada ya ushindi huo mzito, Frank aliwashukuru wanachama wote kwa kujitokeza kwa wingi na kufanikisha sherehe hizo za kufunga mwaka na uchaguzi na pia aliwapongeza wengine waliochagulia katika bodi yake ya chama hicho na kuhaidi watafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na kuwahaidi kuongeza jitihada za kuwakutanisha Watanzania hao na kusaidiana kwa kila hali!

Kwa upande wa msaidizi wa Frank yaani nafasi ya ukatibu ilikwenda kwa Louis ambaye ni mtoto wa mfanyabiashara mkubwa Tanzania Bw. S.H Amoni.

Ifuatayo ni orodha ya matokeo rasmi ya kura yalivyokuwa

MWENYEKITI (RAISI WA JUMUIYA)
Frank Mtao                 55
Christopher Banda     6

KATIBU
Louis Amoni               42
Halima Haule             13
Christopher Banda      6

MWEKA HAZINA
Halima Haule             35
Nadhifa M. Mwinyi     10

WAJUMBE 5 WA KAMATI KUU
Andrea Mburuja        23
Nadhifa M. Mwinyi    22
Fina Nyongo              22
Shomari Abdallah     21
Attu Mwakyusa          19 Waliopita

Henry Maembe         18
Farida P. Banda        12 

Kwa habari zaidi zinapatikana kupitia Facebook ya jumuiya hiyo 

No comments:

Powered by Blogger.