mtuhumiwa wa mauaji auawa na wananchi makete
Na Edwin Moshi, Makete.
Katika
hali isiyo ya kawaida wananchi wanaodhaniwa kuwa ni wa kijiji cha
Usagatikwa kata ya Tandala wilaya ya Makete mkoani Njombe wameamua
kuchukua sheria mkononi kwa kumpiga hadi kumuua Bw. Festo Sigala(44) kwa
tuhuma za mauaji
Tukio
hilo limetokea Septemba 29 mwaka huu katika kijiji cha Tandala wilayani
hapo, baada ya wananchi hao kumfuata mtuhumiwa huyo kwa lengo la
kumdhuru kutokana na tuhuma za mauaji ya mwananmke aliyetambulika kwa
jina la Furaha Datovu Sanga(37)
Akizungumzia
sakata hilo ofisini kwake Mkuu wa polisi(OCD) wilaya ya Makete Alfred
Kasonde (Pichani) amesema Bw. Nesco Thobias Chaula mkazi wa kijiji cha
Usagatikwa aligundua kupatikana kwa mwili wa marehemu Furaha ambaye
aliripotiwa kupotea tangu Mei 15 mwaka huu ambapo alitafutwa bila
mafanikio ambapo mwili huo wa marehemu ulikutwa ndani ya choo cha shimo
kinachomilikiwa na Festo Sigala ambaye kwa sasa ni marehemu
Amesema
baada ya hapo wananchi waliamua kumsaka mtuhumiwa huyo ambapo walimkuta
eneo la stendiya mabasi katika kijiji jirani cha Tandala wakati
akijaribu kutoroka baada ya kupata taarifa kuwa wamegundua kama alifanya
mauaji, na wakaanza kumpa kipigo
"Walimkuta
stendi huyo mtuhumiwa akiwa anataka kutoroka baada ya kujua kuwa
anatuhumiwa kwa mauaji na mwili wa marehemu ulikutwa kwenye choo chake
na wakaanza kumpiga kwa mawe, fimbo wakati alipotaka kutoroka eneo hilo"
alisema Kasonde
Kufuatia
kipigo cha wananchi hao kuwa kikali, mtuhumiwa huyo aliamua kutimua
mbio kuelekea kituo cha polisi Tandala kwa lengo la kujisalimisha,
lakini wananchi hao waliendelea kumfukuza na wakafanikiwa kumzingira na
kuendelea kumshambulia kwa kipigo hasa maeneo ya kichwani amapo ubongo
na damu vilimwagika kwa vingi hadi alipofariki dunia kabla hajafika
kwenye kituo cha polisi
Amesema
kutokana na wingi wa wananchi hao walioamua kujichukulia sheria
mkononi, polisi waliokuwa kazini katika kituo hicho walizidiwa nguvu na
kundi hilo la watu hivyo kushindwa kumnusuru mtuhumiwa huyo asiuawe
kwani nguvu ya wananchi ilikuwa ni kubwa
hata
hivyo baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa marehemu huyo
aliuawa akiwa ndani ya kituo hicho cha Polisi baada ya wananchi kuwazidi
nguvu polisi na kuvinja chumba alichokuwepo marehemu, lakini suala hilo
limekanushwa na OCD Kasonde na kusema kuwa kituo hicho kipo salama na
wala marehemu hakuuawa kwenye kituo cha polisi
"Hakuna
ukweli wowote wa taarifa kuwa ameuawa akiwa lokapu ya kituo cha polisi
Tandala, hakuna kituo kilichovunjwa na badala yake wananchi wenye hasira
kali ndio waliomuua wakati akikimbilia polisi kunusuru maisha yake"
alisema OCD Kasonde
Katika
hatua nyingine ameiomba jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria
mkononi kwani ni kosa kisheria na badala yake wakimkamata mtuhumiwa
wanatakiwa kumfikisha polisi ili sheria ichukuliwe
hadi sasa hakuna anayeshikiliwa kuhusiana na mauaji hayo na uchunguzi bado unaendelea
No comments:
Post a Comment