WAKAZI WA KIKUYU KUSINI WAANDAMANA KUPINGA BOMOABOMOA ILIYOPANGWA NA CDA MKOANI DODOMA, MKUU WA MKOA AINGILIA KATI
Maelfu ya Wananchi wa Kata ya
kikuyu kusini wakiandamana katika mitaa ya mji wa Dodoma kwa ajili ya
kupinga kubomolewa na mamraka ya ustawishaji makao makuu [CDA]
wanaotarajia kubomoa nyumba, mapagale na misingi ya wakazi hao.
Maelfu ya Wananchi wa Kata ya
kikuyu kusini wakiandamana katika mitaa ya mji wa Dodoma kwa ajili ya
kupinga kubomolewa na mamraka ya ustawishaji makao makuu [CDA]
wanaotarajia kubomoa nyumba, mapagale na misingi ya wakazi hao.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema
Nchimbi akipaza sauti ya matumaini kwa wakazi wa Kata ya kikuyu kusini
walioandamana kupinga Bomoabomoa ya CDA waliokuwa wamepanga kubomoa
nyumba na misingi katika eneo hilo. Alisema “Naitengua amri hiyo na
namwagiza Mkurugenzi akutane na wananchi hawa pamoja na viongozi wao ili
kuweza kufikia muafaka kwani kubomoa sio suluhu hamuwezi kubomoa Dodoma
nzima na ningependa kuletewa taarifa juu ya sula hili … mnachotakiwa ni
kuboresha na kutumia njia sahihi ambazo hazita waumiza wananchi ambao
ndiyo wateja wenu.
Diwani wa kata ya Kikiyu kusini
Ancelmu Kutaka akifafanua jambo mbele ya Wananchi wa kata hiyo
waliondamana kupinga kubomolewa na Mamraka ya ustawishaji makao makuu
[CDA] walipanga kuboa wakati wowote kuanzia leo.
Kaimu Mkurugenzi wa CDA Paskas
Mulagili Akifafanua jambo wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa
Habari wa vyombo mbalimbali kuhusu maandamano ya wananchi wa kata ya
Kikuyu Kusini walioandamana kupinga ubomoaji unaotarajiwa kufanywa na
mamlaka hiyo siku yoyote kuanzia leo.
Habari na picha na John Banda, Dodoma
WAKAZI wa Kata za Kikuyu Kusini na
Kilimani mkoani Dodoma wameandamana kupinga amri iliyotolewa na Mamlaka
ya Ustawishaji ya Makao Makuu (CDA) ambayo inawataka kuhama katika eneo
hilo ndani ya siku saba. Wakazi hao walioandamana kutoka Kikuyu hadi
Viwanja vya Nyerere Square katikati ya mji wakimtaka mkuu wa Mkoa wa
Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi kuzungumza nao.
Maandamano hayo yalisindikizwa na ulinzi wa polisi hadi katika viwanja hivyo huku wakazi hao wakiwa wameshikilia mabango yenye jumbe mbalimbali. Wakazi hao wakiwa wanaimba nyimbo huku wakiinua mabango yao juu yenye ujumbe kama Cda ni zaidi ya Alshababi, CCM mnaiona bomoabomoa, Cda ni zaidi ya Nduli Idd Aminini Dada na lingine likisomeka Hata wanyama hupewa hifadhi.
Wakizunguza na waandishi wa habari katika viwanja hivyo wakati wakimsubiri mkuu wa mkoa baadhi ya wananchi na viongozi wao wa mitaa walidai kuwa lengo la maandamano hayo ni kufikisha kilio chao kwa serikali ya mkoa. Andrew Mdumi mwenyekiti wa mtaa wa Mkalama ambao ni sehemu ya eneo linalotakiwa kuvunjwa alisema kuwa wameamua kufanya maandamano hayo mara baada ya kupewa amri ya kuondoka katika eneo wanaloishi kwa kipindi kirefu.
Mdumi alisema, kuwa Mamlaka ya ustawishi Makao makuu imekuwa ikiwapatia namba kila wakati na kudai kuwa itakuja kuwapimia lakini katika hali ya kushangaza imewapa amri ya kuondoka ndani ya siku saba kwa madai kuwa wamevamia katika eneo hilo ambalo lilikuwewa limetengwa kwajili ya bustani za mbogamboga na matunda. “Wanataka tuondoke ili kupisha kilimo cha mbogamboga na matunda hivi kweli mboga na maisha yetu kipi cha msingi kuna nyumba zaidi ya 1000 ambazo watakakuzibomoa kwajili tuu ya kupisha bustani” alisema
Alisema kuwa wamekuwa wakishirikiana na CDA kwa kipindi kirefu ili kuweza kufanikisha zoezi la upimaji wa viwanja hivyo hata kwa gharama zao wenyewe. Mwekiti wa kamati ya upimaji katika Kata ya Kikuyu kusini Mathew Ndallu, alisema kuwa katika kufuatilia suala hilo la kupimiwa viwanja walikutana na CDA na kukubaliana kuwa waje wafanye utambuzi wa nyumba zilizopo, mapagale na misingi ili waweze kufanya upimaji.
Ndallu alisema kuwa walikubaliana
na kuwa kutokana na eneo hilo kuwa halijapimwa wao wako tayari kuchangia
gharama za upimaji ili kuwezesha zoezi hilo kufanyika.
“Tulikubaliana nao mara baada ya
wao kuja kutambua idadi ya nyumba mapagale na misingi watupimia na sisi
tuko tayari kuchangia kiasi cha sh.500,000 kwa kila mwenye eneo” alisema
Ndalllu. Aidha alisema kuwa katika hali ya kushangaza pale ambapo
walikuwa wanasubiri kupimiwa CDA waliwageuka na kuwataka kwanza wao
wapatiwe viwanaja 500 ili waweze kuwapiamia. “Mara baada ya kukubaliana
nao kuwa tuko tayari kuchangia lakini Mkurugenzi alituambia kwanza
tuwape wao viwanja 500 ili waweze kuja kutupimia na kama hatutakubali
basi watakuja kutubomolea” alisema.
Alisema kuwa mara baada ya wao kukataa kumpa mkurugenzi huyo viwanja hivyo aliwaandikia barua hiyo ambayo ilikuwa inawataka wakazi wa maeneo hayo kuondoka kabla ya tarehe 30 ya mwezi Septemba (jana).
“Walituandikia barua ambayo
inatutaka kuaondoka ndani ya siku hizo saba ikiwa ni kuanzia tarehe 23
ya mwezi huu ambapo inaishia leo (jana) na kesho (leo )wanakuja kuanza
kubomoa” alisema Ndallu.
Alisema kutokana na hali hiyo
ambayo imeonyesha kuwa CDA imeshindwa kuwasikiliza kilio chao wameona
kuwa hiyo ndiyo njia sahihi ya wao kupata suluhu ya tatizo lao. Alisema
kuwa jumla ya mitaa mnne katika kata hizo ndiyo inayotakiwa kubomolewa
ambayo ni mitaa ya Mkalama, Chidachi pamoja na Image A na B.
Akizungumza na kundi la wakazi hao mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk Rehema Nchimbi, alisema kuwa anatengua amri hiyo iliyotolewa na CDA na kumtaka Mkurunzi wa mamlaka hiyo kukutana na viongozi wa maeneo husika.
“Naitengua amri hiyo na namwagiza
Mkurugenzi akutane na wananchi hawa pamoja na viongozi wao ili kuweza
kufikia muafaka kwani kubomoa sio suluhu hamuwezi kubomoa Dodoma nzima
na ningependa kuletewa taarifa juu ya sula hili … mnachotakiwa ni
kuboresha na kutumia njia sahihi ambazo hazita waumiza wananchi ambao
ndiyo wateja wenu.
No comments:
Post a Comment