Header Ads

CCM MKOA WA MBEYA YAWAUNGA MKONO WAFANYABIASHARA WALIOGOMEA MASHINE ZA TRA MKOANI MBEYA.

  Mbunge wa Mbozi Mashariki na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya Godfrey Zambi akihutubia mkutano wa hadhara mjini Vwawa.
Meneja wa TRA Wilaya ya Mbozi Ndg. Deo akifafanua jambo mbele ya Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mashariki na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Mhe. Godfrey Zambi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mhe. Elick Ambakisye akiwasalimia wananchi wa mji wa Vwawa.
                     Mzee Mwampamba akitoa salamu za wazee wa mji wa Vwawa.
Mbunge wa Mbozi Mashariki na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya Mhe. Godfrey Zambi akisisitiza kitu kwenye mkutano wa hadhara mjini Vwawa.




Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya na Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mashariki Mhe. Godfrey Zambi amewaunga mkono wafanyabiashara wa Mkoa wa Mbeya kuendelea kugomea kununua mashine za TRA, kutokana na mkanganyiko wa bei za mashine hizo. Mwenyekiti Zambi alisema mashine hizo za TRA Dubai zinauzwa kati ya Dora 50 mpaka 150 yaani wastani wa Shs 240,000/-
Cha kushangaza mashine hizo wafanyabiashara wanauziwa Shilingi 800,000/- kitu ambacho hakikubaliki kabisa. Nae Meneja wa TRA Wilaya ya Mbozi Ndg. Deo alipoitwa kutoa maelezo katika mkutano huo alisema, Mashine hizo haziuzwi na TRA bali zinauzwa na wafanyabiashara walioteuliwa na TRA na wanatekeleza sheria iliyotungwa na bunge inayowataka wafanyabiashara wenye mtaji wa zaidi ya Sh. Milioni 14. Kutumia mashine hizo kutolea risiti kwa wateja.

                                                    Picha zote na Bashiru Madodi
                                                               Basahama blogspot

No comments:

Powered by Blogger.