Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya,(CCM) Dr. Mary Mwanjelwa,
akizungumza na wazazi wa wanafunzi wa shule ya Msingi Airport, Jijini Mbeya
ambako alichangia mifuko 20 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa choo cha wanafunzi
kama alivyoombwa na uongozi wa shule hiyo.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary
Mwanjelwa(kushoto), akikabidhi mifuko 20 ya saruji kwa uongozi wa shule ya
Msingi Airport, Jijini Mbeya kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya wanafunzi wa shule
hiyo kama alivyoombwa na uongozi wa shule hiyo.
Kulia ni diwani wa kata ya Iyela Jijin Mbeya, ndugu
Charles(Chadema), akisalimiana na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya(CCM), Dr.
Mary Mwanjelwa alipofika katika shule ya Msingi Airport, shule ambayo ni pacha
wa shule ya Msingi Pambogo, ambayo alisoma mwana mziki nguli, Tabia Mwanjelwa,
ambaye ni shangazi wa Mbunge, Dr. Mary Mwanjelwa.
Wanafunzi hoyeeeeeeeeeee.......
Baadhi ya walimu wa shule ya Msingi Airport, wakimsikiliza
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya(CCM),Dr. Mary Mwanjelwa, alipofika shuleni
hapo kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa choo cha wanafunzi ambapo alitoa mifuko
20, ya saruji.
Kulia ni Mbunge wa viti maalum wa mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa,
baada ya kuchangia mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa choo cha
wanafunzi wa shule ya Msingi Airport ya Jijini Mbeya, akisalimiana na
Mwalimu''shujaa'',Damari Fidelis Obadia, ambaye ilielezwa kuwa ni Mwalimu pekee
ambaye alichangia Tsh.100,000 kwa ajili ya ujenzi wa choo hicho cha wanafunzi
wa shule hiyo.
''Mungu awabariki'' Mbunge wa viti maalum wa mkoa wa Mbeya, Dr.
Mary Mwanjelwa, akisalimiana na wanafunzi wa shule ya Msingi Airport ya Jijini
Mbeya, alipofika kuchangia ujenzi wa choo cha wanafunzi ambapo alichangia
mifuko 20 ya Saruji.
No comments:
Post a Comment