IRINGA MJINI WASHINDWA KUJITOKEZA KUMSIKILIZA MBUNGE MSIGWA LEO ,MWENYEWE ATOA RAI KWA KIKWETE KUWAFIKISHA MAHAKAMI MAJANGILI
mwakilishi
kutoka shirika la hifadhi la nyanda za juu kusini Godwell ole
meing`ataki wa pili kushoto akiwa na waziri kivuli wa maliasili na
utalii mbunge Peter Msigwa ambae alikuwa mgeni rasimi leo katika
maadhimisho ya Tembo Duniani
Hawa ndio waliofika kumsikiliza
mbunge Msigwa leo uwanja wa historia wa Mwembetogwa ambao kawaida
huwa anajaza umati wa watu ila leo patupu
Wananchi wa jimbo la Iringa mjini wakimsikiliza mbunge Msigwa
mwakilishi
kutoka shirika la hifadhi la nyanda za juu kusini Godwell ole
meing`ataki kushoto akiwa na waziri kivuli wa maliasili na utalii
mbunge Peter Msigwa ambae alikuwa mgeni rasimi leo katika
maadhimisho ya Tembo Duniani
waigizaji wakiigiza jinsi majangili wanavyofanya ujangili
magari ya wadau waliofikia kumsikiliza mbunge Msigwa leo
KWA
mara ya kwanza mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter
Msigwa amevunja rekodi ya kuhotubia wananchi wachache kuliko
mihadhara mbali mbali aliyopata kuifanya katika uwanja wa Mwembetogwa
mjini Iringa .
Uwanja
huo ambao ni uwanja wa Histori kwa mbunge Msigwa kupata
wasikilizaji wengi jana amejikuta akiambulia patupu baada ya idadi
ya watu waliofika kumsikiliza kufika idadi ya chini ya 30 jambo
ambalo limezua maswali mengi zaidi.
Pamoja
na kuwa mhadhara huo wa leo haukuandaliwa na Chadema bali ulilenga
kuadhuimisha siku ya Tembo Duniani ila bado kwa kiasi mvuto wa
maadhimisho hayo yamepoteza mwelekeo .
Baadhi
ya wadau waliozungumza na mtandao huu wamedai kuwa waandaaji wa
maadhimisho hayo ya siku ya Tembo Duniani ndio ambao wamefanya
maadhimisho hayo bila kujiandaa na ndio sababu ya wananchi kupuuza
kufika uwanjani hapo.
Kwa
upande wake mbunge Msigwa alimtaka Rais Jakaya Kikwete kuwachukulia
hatua wale wote wanaotajwa kujihusisha na ujangili wa meno ya
tembo ambao waziri wa maliasili na utalii amekuwa akieleza umma kuwa
watu hao wanajulikana .
Msigwa
aliwataka wananchi wa nyanda za juu kusini kufichua majangili wa meno
ya tembo ili kuendeleza utalii na kujipatia kipato.
Kauli
hiyo ameitoa leo wakati wa maadhimisho ya kupinga uuaji wa tembo
dunuani ambayo yamefanyika mkoani Iringa yenye kauli mbiu inayosema
pinga ujangiri,na kubainisha kuwa utalii bila tembo hakuna utalii.
"Napenda
kutoa rai kwa kupitia hadhara hii kumshinikiza Raisi wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kwa dhamana
aliyopewa kwa kupitia katiba, aweze kuwafikisha mbele ya vyombo vya dola
na kuwatendea ipasavyo watuhumiwa wote wa ujangili hasa wa
tembo....Natoa shinikizo hili kwa kuwa mara kadhaa, mawaziri wenye
dhamana wameendelea kukiri kuwa wanawafahamu majangili mpaka sehemu
wanazokaa lakini imeendelea kuwapa muda. Swali la kuuliza, je tunasubiri
tembo watoweke ndio tuanze kumtafuta mbaya/mchawi wetu? Ama ndo msemo
wa waswahili kuwa 'La kuvunda halina ubani?'"
Msigwa
alisema kuwa moja kati ya maazimio katika maadhimisho ya siku ya
tembo ni pamoja na kumtaka Raisi kuwachukulia hatua maafisa na
watendaji wote wa Serikali na vyombo vya usalama ambao kwa muda mrefu
wamekuwa wakishukiwa na kushutumiwa kwa ushiriki wao hasa katika kulinda
ama kusaidia mtandao wa ujangili nchini.
Alisema
kuwa Rais Kikwete hana budi kulichukulia jambo hili la ujangili wa
tembo kwa uzito mkubwa na kulipa nafasi katika moja ya mambo ya msingi
ambayo kama Taifa lazima tuyazungumze bila kificho wala kulinda maslahi
ya watu wachache tena kwa uwazi na ukweli kwa kushirikiana na umma wa
watanzania.
Hata
hivyo alisema hadi sasa ni dhahiri kuwa ukimya wa Serikali na
kigugumizi chake cha kuwachukulia hatua watuhumiwa kunatokana na
ubinafsi, uozo na kutojali maslahi ya taifa kwa ujumla.
"...Napenda
kuwahakikishia waandaji kuwa , nitaendelea kuwa mstari wa mbele katika
kulinda rasilimali hizi muhimu na urithi huu mkubwa wa taifa letu kwa
moyo wangu, nafsi yangu,nguvu zangu na akili zangu kwa kushirikiana na
watanzania wote kwa ujumla bila kujali tofauti za kiitikadi na
misimamo...ningependa kuongea mengi, ila kwa leo napenda kumalizia kwa
kuwakumbusha wananchi pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali kuendelea
kutimiza wajibu wake wa kulinda haki za wanyamapori hasa tembo hata
pale tunapoona kuwa Serikali inafanya jitihada hafifu katika mambo ya
msingi.
kwa upande wake mwakilishi kutoka shirika la hifadhi la nyanda za juu kusini Godwell ole meing`ataki amesema kuwa Serikali inachangia billion 11 katika kuendeleza miradi ya wananchi kama maji elimu,miradi ya kijamii na na kimazingira ambayo fedha hizo zinatoka katika mfuko wa utalii na maliasili.
Meing`ataki
amewaomba wananchi pia kuwafichua wmajangiri wa tembo ili kusaidia
watalii waweze kuja nchini na kujipatia kipato ili nchi iweze kuendeleza
miradi ya kijamii.
Serikali
kwa kutimiza wajibu wake wa kudhibiti biashara haramu ya wanyamapori ni
lazima pia mashirika yasiyo ya kiserikali kuendelea kuongeza juhudi zao
kuhakikisha kuwa elimu kutolewa kwa umma ili kuongeza nguvu ya pamoja
katika masuala ya kulinda wanyamapori.
No comments:
Post a Comment