WIZARA YA AFYA YAPOKEA MAGARI 2 YA KUBEBEA WAGONJWA KUTOKA KWA WADAU WA AFYA WA AUSTRALIA KUSAIDIA HOSPITALI YA KISARAWE
Kaimu Katibu mkuu wa Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii Bi.Regina Kikuli akiongea na waandishi wa habari
(hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada wa magari 2 ya
kubebea wagonjwa kutoka kwa wadau wa afya wa Australia.
Muuguzi mkuu wa Idara ya Afya
kutoka serikali ya Australia Bi. Catherine Stoddart (kushoto)
akimkabidhi funguo za magari ya kubebea wagonjwa Kaimu Katibu mkuu wa
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi.Regina Kikuli katika viwanja vya
wizara hiyo jijini Dar es salaam. Magari hayo 2 yaliyotolewa kwa msaada
wa wadau wa afya wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya Austaralia
yatapelekwa kusaidia utoaji wa huduma za afya ya mama na mtoto katika
hospitali ya wilaya ya Kisarawe.
Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii Bi.Regina Kikuli(kulia) akiwaonyesha waandishi wa habari
(hawapo pichani) funguo za magari mawili ya kubebea wagonjwa
aliyokabidhiwa na wadau wa mashirika yasiyo ya serikali kutoka
Austaralia.
Wawakilishi wa wadau wa afya
mashirika yasiyo ya serikali kutoka Austaralia wakiongozwa na Muuguzi
mkuu kutoka Idara ya Afya ya serikali ya Australia Magharibi Bi.
Catherine Stoddart (wa pili kutoka kushoto waliokaa) wakiwa katika picha
ya pamoja na baadhi ya watendaji wa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
mara baada ya kukabidhi msaada wa magari 2 ya kubebea wagonjwa. Picha na
Aron Msigwa – MAELEZO.
No comments:
Post a Comment