UN YAENDESHA SEMINA YA MAFUNZO JUU YA HAKI ZA BINADAMU KWA WAANDISHI WA HABARI NCHINI.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa
Mataifa Tanzania Hoyce Temu akitoa muhtsari kwa waandishi wa habari juu
ya Taarifa kuhusu Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Msaada wa Maendeleo
UNDAP 2011-2015 ambao unaelezea ushiriki wa Umoja wa Mataifa katika
kuendeleza nyanja mbalimbali ikiwemo kupunguza umaskini wakati wa Semina
ya kuwapa uelewa waandishi wa habari juu ya Haki za Binadamu tukielekea
kwenye maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani
itakayoadhimishwa tarehe 10 Disemba mwaka huu.
Mwezeshaji wa Semina hiyo Katibu
wa Jukwaa la Wahariri nchini Neville Meena akitoa changamoto kwa
wanahabari kutumia fursa mafunzo hayo katika kuhabarisha jamii kuhusu
kazi zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini.
Mwakilishi Msaidizi wa UNICEF Bw.
Paul Edwards akielezea nia ya Umoja wa Mataifa kuwakutanisha waandishi
wa habari kila mwaka katika semina za mafunzo ambapo amesema jitihada za
Umoja huo kutoa mchango katika juhudi endelevu za kupunguza umaskini na
kupatikana kwa haki za Binadamu kulingana na visheni ya Maendeleo ya
Taifa la Tanzania.
Mtalaam wa Program wa UNDP Bw.
Amon Manyama akiwasilisha kwa wanahabari mpango kazi maalum wa miaka
minne unaojulikana kama United Nations Development Assistance Plan
2011-2015 (UNDAP) uliotenga dola za Kimarekani Milioni 777 kwa Serikali
ya Tanzania mpaka kukamilika ifikapo 2015.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa yasiyo na ukazi hapa nchini Bi. Aine Mushi akizungumzia jinsi
mashirika hayo yanvyoweza kufanya kazi kwa pamoja 'Delivering As One' na
Mashirika ya Umoja wa mataifa yenye ukazi hapa nchini.
Pichani Juu na Chini ni Washiriki
wa Semina ya siku moja kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki
za Binadamu na Utawala Bora Mh. Mahfoudha Alley Hamid akizungumzia haki
za msingi za Binadamu na wajibu wa vyombo vya habari katika kutetea
haki hizo na kufichua pale zinapokiukwa ikiwemo kufuata maadili.
Afisa Mipango Mwandamizi wa
Shirika la Kazi Duniani (ILO) Bw. Anthony Rutabanzibwa akitoa somo jinsi
waandishi wa habari wanavyotakiwa kuripoti masuala yanayohusu hakiza
Binadamu bila kutoka nje maadili ya kazi zao.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya
washiriki wakichangia mada na kutoa maoni wakati wa semina hiyo.
Mwenyekiti wa timu ya Mawasiliano
ya Umoja Mataifa Bw. Yusuph Al Amin wakati wa semina hiyo akifafanua
jinsi sekta ya mawasiliano vikiwemo vyombo vya habari inavyoweza
kuchangia maendeleo na kufanikisha kufuatwa kwa haki za binadamu.
Afisa habari wa kituo cha habari
cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi.Usia Ledama akitoa changamoto kwa
wanahabari kusoma makabrasha yanayotolewa na mashirika mbalimbali ya
umoja wa mataifa wakati wa mikutano na semina za kuelimishana kuhusiana
na masuala mbalimbali yanayohusu jamii kwani kwa kufanya hivyo ndivyo
watakavyoeweza kuelewa ushiriki wa Umoja wa Mataifa katika kupunguza
umaskini na kutetea haki za binadamu.
Baadhi ya Maofisa wa Umoja wa
Mataifa na Wanahabari wakati wa Semina hiyo.
No comments:
Post a Comment