MKURUGENZI MKUU WA EABC AKUTANA NA WANAHABARI WA EAC KATIKA MAFUNZO
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la
Biashara la Jumuia ya Afrika Mashariki, Andrew Luzze Kaggwa, akizungumza
wakati wa mafunzo ya siku tatu ya waandishi wa habari juu ya Wajibu wa
Vyombo vya Habari katika kuangalia Utekelezaji wa Masuala ya Soko la
Pamoja. Mafunzo hayo yanahusisha wanaandishi wa habari kutoka nchi zote
wanachama wa EAC, na kufanyika Ubungo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la
Biashara la Jumuia ya Afrika Mashariki, Andrew Luzze Kaggwa, akizungumza
wakati wa mafunzo ya siku tatu ya waandishi wa habari juu ya Wajibu wa
Vyombo vya Habari katika kuangalia Utekelezaji wa Masuala ya Soko la
Pamoja. Wengine pichani ni washiriki wa mafunzo hayo.
Katibu wa baraza la Asasi za
Kijamii la Jumuia ya Afrika Mashariki, Dk. Martin Mwodha, akizungumza
katika mafunzo hayo juu ya ushiri wa Asasi za kiraia katika ulelimishaji
na ufikishaji wa elimu ya Soko la Pamoja la EAC.
Mchambuzi wa Siasa za Afrika
ambaye pia ni Mwanahabari Mkongwe nchini Tanzania, Jenerali Ulimwengu
akitoa mada katika mafunzo hayo leo.
Dawati la ufundi nalo wakati wote
lilikuwa katika wakati mgumu wakuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.
Kutoka kushotoni Aline Ellermann, Elizabeth Wanyoike na Hussein Karim
wote kutoka ofisi ya GIZ ambao ndio wawezeshaji mafunzo hayo
yaliyoandaliwa pamoja na AC
Kuna wakati mambo yanaonekana
hayaendi na hapa anaonekana Elizabeth Wanyoike (kulia) akikuna kichwa)
huku Aline Ellermann akiendelea na kazi.
Fiona Mbabazi kutoka Rwanda
akimshukuru Ofisa mtendaji wa EABC, Andrew Kaggwa kwa maelezo juu ya
Baraza hilo.Kati ni Jenerali Ulimwengu na Aline Ellermann.
Bizimana Jean-Marie akitoa zawadi
kwa Dk. Martin Mwadha wa Asasi za Kiraia za EAC, wengine pichani kutoka
kushoto ni Elizabeth Wanyoike wa GIZ, Balozi Jeremy Ndayiziga, Andrew
Kaagwa na Jenerali Ulimwengu.:Picha zote na Mroki Mroki wa Father Kidevu
Blog
No comments:
Post a Comment