NMB KUANZA KUKOPESHA WANANCHI NYUMBA ZA BEI NAFUU
Mahmoud Ahmad Arusha
WADAU mbalimbali wa benki ya NMB
mkoani Arusha wameiomba benki hiyo kuanzisha utaratibu wa kuwakopesha
wateja wake nyumba za gharama nafuu ili kuwanufaisha na mikopo
wanayokopa katika benki hiyo hususani wajasiriamali wenye kipato kidogo.
Pamoja na kuwa benki hiyo imekuwa
ikitoa mikopo ya aina mbalimbali kwa wateja wake , hali hiyo
imewawezesha kuwaondoa katika wimbi la umaskini kwa kuanzisha miradi
midogomidogo, ila kwa upande wa nyumba imekuwa ni changamoto kubwa kwao
kwani bado benki hiyo haijaweza kuwasaidia .
Hayo yalielezwa na wafanyabiashara wananchama wa klabu ya NMB (NMB Business Club,)mkoani
hapa,wakati walipohudhulia mafunzo ya pili ya siku moja ya
ujasiriamali yanayotolewa na benki hiyo kupitia virabu vya wajasiriamali
vya NMB,ambapo mwaka huu yanayolenga kujua faida na athari za ushindani
katika biashara zao yaliyofanyika jijini hapa.
Alisema kuwa, asilimia kubwa ya
wadau wa benki hiyo wamekuwa wakichukua mikopo kwa ajili ya kuboresha
biashara zao ila wengi wao bado hawajaweza kujenga nyumba nzuri za
kuishi hususani wenye vipato vya chini, hivyo endapo benki hiyo
itaanzisha mchakato wa kuwajengea na kuwakopesha nyumba za bei nafuu
wataweza kuwasaidia kuondokana na changamoto hiyo.
‘Kwa kweli benki hii imekuwa
ikitusaidia sana sisi wajasiriamali katika kuhakikisha tunajikwamua
na biashara na kuweza kuondokana na changamoto mbalimbali za kimaisha ,
hivyo endapo watatujengea nyumba hizo za bei nafuu tutaweza kuishi
maisha yaliyo bora zaidi’alisema Amina.
Aidha waliiomba benki hiyo
,kuanzisha huduma za viza kama wanavyofanya benki nyingine ili
kuwawezesha kuchukua fedha hata wawapo nje ya nchi ili kuweza kufanya
bishara zao kwa uhakika zaidi wawapo nje ya nchi.
Akifungua mafunzo hayo , Meneja
wa benki hiyo kanda ya kaskazini Vicky Bishubo alisema kuwa benki hiyo
imeboresha huduma ya mikopo kwa wajasirimali kwa kiwango kikubwa kutoka
shilingi milioni 1 na milioni 5 hadi kufikia sh, milioni 10 , hatua
ambayo alisema itamsaidia mfanyabiashara mdogo kuongeza biashara zake na
kujitanua zaidi.
Alisema kuwa , mafunzo hayo
ambayo yamekuwa yakitolewa mwaka hadi mwaka yamekuwa yakiwawezesha
wajasirimali hao kuboresha biashara zao ikiwa ni pamoja na kubuni
biashara mpya zenye tija ambazo zimewawezesha kujikwamua kiuchumi.
Bishubo alitaja malengo ya
mafunzo hayo ni kuwawezesha washiriki kupata magfunzo ya msingi ya
usimamizi wa biashara ,kuwawezesha washiriki kuelewa maana ya
ujasirimali na kupata mbinu za kufanikisha biashara ba kuiendeleza
,pamoja na kuwawezesha kuwa na ujasiri wa kuchukua mikopo.
Naye Mkuu wa kitengo cha
wajasiriamali , Filbert Mponji alisema kuwa,benki hiyo imejiwekea
mkakati ifikapo mwaka 2013 kuanzisha akaunti ya biashara kwa
wajasirimali itakayowawezesha kuchukua fedha wakati wowote wanapohitaji.
No comments:
Post a Comment