Header Ads

RAIS KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA SEKTA YA AFYA IKULU, APOKEA CHETI CHAKE CHA UDAKTARI WA MUHASRAIS KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA SEKTA YA AFYA IKULU, APOKEA CHETI CHAKE CHA UDAKTARI WA MUHAS

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea  toka kwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Prof. Ephata Kaaya Cheti cha Udaktari wa Public Health (Honoris Causa), kufuatia Shahada aliyotunukiwa na Chuo hicho mwaka  2010 kwa Kutambua mchango wa Rais Kikwete katika kuendeleza Sekta ya Afya nchini. Sherehe hiyo fupi ilifanyika leo Novermba 23, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam.
 Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Prof. Ephata Kaaya akisoma risala kabla ya kumkabidhi Rais Kikwete Cheti cha Udaktari wa Public Health (Honoris Causa), kufuatia Shahada aliyotunukiwa na Chuo Desemba mwaka 2010 kwa Kutambua mchango wa Rais Kikwete katika kuendeleza Sekta ya Afya nchini leo Novermba 23, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam..
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya kumbukumbu na Waziri wa Ardhi Prof Anna Tibaijuka, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi na viongozi wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili baada ya kukabidhiwa  Cheti cha Udaktari wa Public Health (Honoris Causa), kufuatia Shahada aliyotunukiwa na Chuo hicho mwaka  2010 kwa Kutambua mchango wa Rais Kikwete katika kuendeleza Sekta ya Afya nchini leo Novermba 23, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam. 
Rais Jakaya  Mrisho Kikwete  akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa Kampasi ya Afya ya Chuo Kikuu cha Dodoma kutoka kwa Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (National Health Insurance Fund) NHIF Bw. Emmanuel Humba leo Novemba 23, Ikulu jijini Dar es salaam .
 Rais Jakaya  Mrisho Kikwete  katika picha ya kumbukumbu baada ya kupata  maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa Kampasi ya Afya ya Chuo Kikuu cha Dodoma kutoka kwa Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (National Health Insurance Fund) NHIF Bw. Emmanuel Humba leo Novemba 23, Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya  Mrisho Kikwete  na ujumbe wa Wizara ya Afya na  Mfuko wa Afya ya Jamii (National Health Insurance Fund) NHIF Bw. Emmanuel Humba leo Novemba 23, Ikulu jijini Dar es salaam

No comments:

Powered by Blogger.