TBL YASAIDIA UCHIMBAJI VISIMA VYA MAJI MOROGORO
Mkurugenzi wa Uhusiano na
Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto)
akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 24.9 Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, Dk. Ntobi Mwakibete za
kusaidia kuchimba kisima cha maji. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa
wiki mjini Morogoro.
Mkurugenzi wa Uhusiano na
Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto)
akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 26.7, Meya wa
Manispaa ya Morogoro, Amiri Nondo kwa ajili ya mradi wa maji kwa shule
12 za sekondari za manispaa hiyo.Kulia ni Meneja Uendeshaji wa Kampuni
ya Uchimbaji Visima vya Maji ya Jae-Hi-Tech Dry Cleaning, Maximillian
Makota na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Jovis Simbeyi. Hafla hiyo
ilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.
Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amiri Nondo akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 26.7, Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Uchimbaji Visima vya Maji ya Jae-Hi-Tech Dry Cleaning, Maximillian Makota zilizotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa ajili ya uchimbaji wa visima vya maji mkoani humo. Kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.
Ofisa Ustawi Jamii
Sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro, Tabitha Majiku (kulia) akitoa neneo
la shukrani baada ya kupokea msaada wa fedha za kusaidia miradi ya maji
mkoani humo kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika hafla
iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa
Morogoro. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL,
Steve Kilindo na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa
Morogoro, Dk. Ntobi Mwakibete (wa pili kulia).




No comments:
Post a Comment