Jeshi la polisi mkoa wa Iringa limebariki
maandamano ya wanahabari mkoa wa Iringa yaliyopangwa kufanyika
kesho majira ya saa 4 asubuhi katika mji wa Iringa. Katika
kibali hicho kilichotolewa na jeshi la polisi leo asubuhi kabla
ya kutolewa lilikutana na katibu wa IPC Frank Leonard kuomba
kufanya marekebisho ya njia na kukubaliana na kuifuta njia ya
Uhindini na badala yake kuruhusu maandamano hayo kutumia barabara
ya Uhuru kutoka Bustani ya Manispaa ya Iringa kwenda barabara ya
samora na kuishia kanisa la RC mshindo na baada ya hapo kurudi kwa
kupita barabara ya Mashine tatu ,Stendi kuu ,M.R Hoteli na kuishia
ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa. Katika barua hiyo ya jeshi
la polisi yenye kumbukumbu namba IRI/A./14/VOl.x11/178 iliyotumwa
kwa mtendaji mkuu wa Iringa Press Club yenye kichwa cha Maombi ya
kibali cha kufanya maandamano ya amani . Imeanza kwa kusema
tafadhali rejea barua yako kumb. IPC/02/o12/ Machi 2 ya
03/03/2012 inayohusu kichwa cha habari hapo juu. Kibali
kimetolewa cha kufanya maandamano ya amani kwa Klabu ya
wanahabari mkoa wa Iringa mnamo tarehe 6/3/2012 muda wa saa 4
asubuhi kama ifuatavyo maandamano hayo yataanzia kwenye bustani ya
manispaa ya Iringa kuelekea kanisa la Mshindo kwa kupitia barabara
ya Uhuru. Baada ya kufika kanisa la Mshindo watapita barabara
ya Ubena Club kuelekea stendi kuu ,MR Hotel,Luxury hadi ofisi za
mkuu wa mkoa ambapo yataishia . Nakala kwa RPC Iringa kwa
taarifa na RTO tafadhali panga askari wa kuongoza maandamano hayo
Nawatakia maandamano mema Mkuu wa polisi wilaya ya Iringa
MOhamed Mkwazu Semunyu
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments:
Post a Comment