Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mohamed Gharib Bilal
akisalimiana na mkurugenzi mtendaji wa Tume ya Kikristo ya Huduma za
jamii Bw. Peter Maduki (kushoto) mara baada ya kufungua mkutano wa
kimataifa unaojadili utoaji wa fedha za miradi ya afya kulingana na
huduma zinazotolewa katika vituo husika vya afya mkutano ambao
umewashirikisha wahisani na wajumbe kutoka nchi 15 za Afrika.Katikati
ni Waziri wa Afya wa Burundi Dkt.Sabine Ntakarutimana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mohamed Gharib Bilal
akiwa katika picha yya pamoja na viongozi wa Wizara ya Afya na Ustawi
kutoka Tanzania na baadhi Jamii na viongozi wafadhili wa
mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa
wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
Washiriki
wa mkutano unaojadili utoaji wa fedha za miradi ya afya kulingana na
huduma za afya zinazotolewa kutoka nchi 15 za Afrika wakiendelea na
mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akiagana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt.Haji Mponda,
baada ya kufungua mkutano wa siku mbili wa Kimataifa wa kujadili na
kubadilishana mawazo kuhusu ufadhili wa miradi yenye ufanisi katika nchi
saba za Afrika Mashariki, ulioanza leo Machi 6, 2012 jijini Dar es
Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Mkutano
wa Kimataifa wa siku mbili wenye lengo la kujadili na kubadilishana
mawazo kuhusu ufadhili wa miradi yenye ufanisi katika nchi saba za
Afrika Mashariki, ulioanza leo Machi 6, 2012 jijini Dar es Salaam.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Reviewed by
crispaseve
on
8:26 AM
Rating:
5
No comments:
Post a Comment