UN YAENDESHA WARSHA KWA MAAFISA MAWASILIANO WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR.
Waziri
wa nchi ofisi ya Rais na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Zanzibar Mheshimiwa Dr. Mwinyihaji Makame akifungua warsha ya maafisa
mawasiliano wa Wizara husika Zanzibar. Katikati ni kaimu mwakilishi wa
UN Zanzibar Bi. Ruth Leano na kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa
Mataifa, Bw. Alberic Kacou.
Kaimu Mwakilishi wa UN Zanzibar Bi. Ruth Leano na naye aliwakilisha program za UN zilizopo Zanzibar.
Mmoja wa watoa mada kuhusu Mpango wa kufanya kazi pamoja kutoka UN Bwana George Otoo akiwasilisha maoni yake.
Mmoja
wa Maafisa Mawasiliano toka serikali ya Zanzibar,Wizara ya Afya
akisisitiza yaliyomo katika Mpnago wa Umoja wa Mataifa wa Msaada wa
Mendeleo (UNDAP).
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Hoyce Temu akiteta na Mheshimiwa Waziri Mwinyihaji Makame.
Baadhi ya Wanamawasiliano wa serikali ya Zanzibar wakifuatilia kwa makini warsha hiyo.
Baadhi ya maafisa mawasiliano wakifuatilia kwa makini warsha iliyoandaliwa na UN.
Picha ya pamoja.
---
---
Shirika
la Umoja wa Mataifa Tanzania kupitia kundi la maafisa mawasiliano
linalojulikana kama United Nations Communication Group (UNCG),
limeendesha warsha ya siku moja mjini Zanzibar kwa maafisa mawasiliano
wa serikali ya Zanzibar wanaofanya kazi katika wizara zote za Zanzibar.
Warsha
hiyo ilihudhuriwa na maafisa 40 wa wizara husika na ilihusu jinsi gani
ya kuwawezesha wanamawasiliano wa serikali ya Zanzibar na UN
kuimarisha mawasiliano yanayohusu maendeleo ya Jamii, hususan ya
Zanzibar.
Mheshimiwa
Dr. Mwinyihaji Makame, waziri wa nchi ofisi ya Rais na mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Zanzibar alifungua warsha hiyo. Julai 2011, UN
pamoja na serikali ya Tanzania ilisaini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa
Msaada wa Maendeleo wa miaka minne (UNDAP).
Mpango
huu umelenga kufanya kazi kwa pamoja na serikali ya Tanzania. Utoaji
wa warsha kwa maafisa Mawasiliano wa serikali ni moja ya mikakati ya
kuimarisha utoaji taarifa wa maendeleo ya programu zinazofanywa kwa
pamoja ambapo kundi la Mawasiliano la UN litakutana na wanamawasiliano
wa bara mwezi ujao.
No comments:
Post a Comment