ZIARA YA DK BILAL WILAYANI NKASI
MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA DAHARIA LA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA YA KORONGWE BEACH-WILAYA YA NKASI.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe
kuzindua rasmi jengo la Daharia la Shule ya Sekondari ya wasichana ya
Korongwe Beach , iliyopo Wilaya ya Nkasi, wakati akiwa katika ziara yake
ya Mkoa wa Rukwa na Katavi, jana Februari 21, 2012. Kulia kwake ni
mkewe Mama Asha Bilal. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la
Msingi katika jengo la Daharia la Shule ya Sekondari ya wasichana ya
Korongwe Beach , iliyopo Wilaya ya Nkasi, wakati akiwa katika ziara yake
ya Mkoa wa Rukwa na Katavi, jana Februari 21, 2012. Kushoto kwake ni
mkewe Mama Asha Bilal. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akinawa maji ya Kisima cha kupampu yanayovunwa kwa mvua,
kilichojengwa katika Kijiji cha Mwamapuli wakati alipokuwa katika ziara
yake ya mkoa wa Rukwa na Katavi juzi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda Mti wa kumbukumbu nje ya jengo
la Daharia la Shule ya Sekondari ya wasichana ya Korongwe Beach ,
iliyopo Wilaya ya Nkasi, baada ya kuzindua Daharia hilo wakati akiwa
katika ziara yake ya Mkoa wa Rukwa na Katavi, jana Februari 21, 2012.
Nyuma yake ni mkewe Mama Asha Bilal na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Eng. Stella Manyanya. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akiwasili kwenye Uwanja wa Korongwe kwa ajili ya kuwahutubia
wananchi wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Rukwa na Katavi jana
Februari 21, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akizungumza na Mkazi wa Kijiji cha Mwamapuli, Yacoub Jilala,
ambaye ni mlemavu, baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi wa kijiji
hicho, alipofika kuzindua jengo la Ghara la mazao, akiwa katika ziara
yake ya mkoa wa Rukwa na Katavi, juzi Februari 20, 2012. Picha na
Muhidin Sufiani-OMR
No comments:
Post a Comment