SERIKALI MKOANI RUVUMA IMESIKITISHWA NA TUKIO LA MAANDAMANO YA VIJANA YASIYO HALALI
Serikali
imesikitishwa na tukio la kundi la Vijana waendesha pikipiki maarufu
kama yebo yebo kufanya maandamano katika Mitaa ya Manispaa ya Songea
na kusababisha vurugu kubwa na uhalibifu wa mali.
Akitoa
tamko hilo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ameeleza kuwa kwa
muda wa siku tatu zilizopita kumekuwepo na tetesi za kutokea mauaji kwa
imani za kishirikina zenye kulenga zaidi akinamama kuondoa sehemu za
mwili kuwasaidia mambo ya kibiashara hivyo kupelekea watu kufariki.
Kufuatia
matukio hayo mkoa uliagiza Jeshi la polisi kuchukua hatua za
kudhibiti hali hiyo kwa kufanya uchunguzi wa wanaojihusisha na mauaji
hayo kazi inayoendelea hadi sasa.
Katika
maandamano ya leo watu wawili wamefariki dunia kwa kupigwa risasi
wakati polisi wakiwatawanya waandamanaji hao waliokuwa wakiwarushia
mawe polisi wa kutuliza ghasia
Aidha
Mkuu wa mkoa amewasihi wananchi wa Songea na Ruvuma kwa pamoja wawe
watulivu katika kipindi hiki kigumu ili vyombo vya ulinzi na Usalama
viendelee kutekeleza jukumu lake la kuhakikisha wote wanaojihusisha na
biashara hii haramu wanachukuliwa hatua za kisheria
Ametoa
wito wananchi kuwabaini watu wanaondesha uhalifu kwa njia ya uchawi
na ushirikina na ambao wanaishi katika Mitaa yetu kwa kutoa taarifa
zao kwa viongozi wa Mitaa na vyombo vya ulinzi na Usalama mapema.
“Serikali
haimini kuhusu ushirikina wala uchawi.Inaelewa kuhusu tiba asilia na
kwa tiba hizi hufanywa na watu wanaopewa vibali na serikali” alisema
na kusisitiza kuwa wananchi wa Ruvuma wakatae ushirikina wa kiwango
hicho pia uendeshaji wa ramli chonganishi zenye lengo la kugombanisha
ndugu,jamii na Taifa kwani madhara yake ni kutokea mauaji kama haya
kwa wasio na hatia.
Mkuu
wa Mkoa ametoa rai kwa wananchi wa Ruvuma kutoa ushirikiano na vyombo
vya ulinzi na Usalama katika kipindi hiki kwa kuwabaini wote
wanaojihusisha na kuendeleza uhalifu huu kwa vigezo vya uchawi na
ushirikiana
Amewaagiza
watendaji wa Mitaa,kata na Tarafa kuhakikisha ulinzi kwa kushirikiana
na Polisi wanaendesha operesheni katika Mitaa yote na nyumba za
kulala wageni ili kuwabaini wahalifu wote huku hatua za kisheria
zikichua mkondo.
“Sote
tukiungana hawa wachawi,waganga wa jadi na majambazi wanaodandia humo
tunaweza kuwadhibiti ili mauaji yakome na Songea irudie utulivu wake
kama kawaida” alisema Mkuu wa Mkoa
Kwa
mujibu wa taarifa za polisi jumla ya watu watano hadi sasa
wameripotiwa kuuwawa kwa hisia za ushirikina na uchawi katika maeneo ya
Lizaboni, Bombambili na Matarawe kati yao wanawake watatu na wanaume
wawili.Hata hivyo kati yao hakuna hata mmoja aliyeondolewa kiungo cha
mwili kama wanavyodia baadhi ya wananchi waliondamana.
Imetolewa na
Revocatus A.Kassimba
Afisa Habari
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma
No comments:
Post a Comment