Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Beatha Swai
MBUNGE
wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mbeya,Hilda
Ngoye na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Beatha Swai wamenusurika kifo
baada ya gari walilokuwamo kugonga pikipiki na kisha kupinduka mtaroni.
Tukio
hilo lilitokea majira ya saa nne asubuhi katika mji wa Chimala wilaya
ya Mbarali ambapo msafara wa katibu huyo pamoja na mbunge walitangulia
mbele kabla ya msafara wa makamu wa raisi kuanza.
Ajali
hiyo ilihusisha gari lenye namba za usajili STK 2429 analotumia katibu
tawala wa mkoa Mbeya na pikipiki ambayo namba zake hazikupatikana
maramoja pamoja na jina la mwendesha pikipiki huyo.
Katika
eneo la tukio kamanda wa polisi mkoani hapa Advocate Nyombi alisema
viongozi hao hawakujeruhiwa isipokuwa mwendesha pikipiki ambaye
alikimbizwa katika hospitali ya misheni ya Chimala kwa ajili ya
matibabu.
Aidha
chanzo cha ajali alisema ni mwendesha pikipiki kugeuza katikati ya
barabara wakati gari la katibu huyo likiwa karibu naye hiyo dereva
alishinwa kulimudu gari lake kisha kutumbukia katika ukingo wa
barabara.Chanzo Mbeya Yetu Blog
No comments:
Post a Comment