Mwili wa Marehemu Esther Badi aagwa leo
Jeneza
la mwili wa marehemu mama Esther Badi ambaye ni mama mzazi wa aliyekuwa
katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Brandina Nyoni, na
Mpigapicha wa Magazeti ya This Day na Kulikoni, John Badi likiwa ibada
maalum ya kuaga mwili wa marehemu iliyofanyika leo kwenye
kanisa kilutheri la Azani Front jijini Dar es salaam leo, mwili wa
marehemu umesafirishwa kwenda mkoani Iringa na utazikwa katika kijiji
cha Ilembula huko Njombe.
Bi. Blandina Nyoni Mtoto wa Marehemu mama Esther Badi akitoa historia ya marehemu wakati wa ibada hiyo leo.
Waombolezaji mbalimbali wakiwa katika ibada hiyo.
Ndugu na jamaa wakiwa katika ibada hiyo leo.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa jamii Dk. Hadji Mponda kulia akiwa pamoja na
Paniel Lyimo katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu wamehudhuria ibada hiyo
pia.
Mwili wa marehemu ukiandaliwa tayari kwa waombolezaji kuanza kutoa heshima zao za mwisho.
Paniel Lyimo katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (kulia)akitoa heshima
zake za mwisho mbele ya jeneza la mwili wa marehemu Mama Esther Badi.
Waombolezaji wakielekea kutoa heshima zao za mwisho.
No comments:
Post a Comment